Katibu Mkuu wa CHADEMA; Dk Wilbrod Slaa.
|
DK. Willbroad Slaa "Sifikirii kuelekeza nguvu zangu kwenye kuwania
urais 2015 wapo watu wengi wenyesifa katika kundi la UKAWA.
Kila kitu kitafanywa
kwa wakati muafaka,kazi iliyopo mbele yangu ni kupigania umoja wetu wa UKAWA ili
kuleta ushindani wa kweli katika uchaguzi 2015.
Akizungumzia hatua ya UKAWA kususia Bunge Maalumu la Katiba Dk. Slaa
alisema umoja huo uko sahihi kwani umesimama upande wa wananchi, ninaheshimu
uamuzi wa Viongozi wangu Mh Freeman Mbowe Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia.
UKAWA imebeba maoni ya wananchi na suala la kutengeneza Katiba sio suala
la rais,serikali wala chama chochote bali ni la wananchi.
Serikali ina viongozi vigeugeu kwa sababu ni wao ndio waliosaini rasimu
ya Katiba mpya, lkn cha ajaabu wao ndio wanageuka na kutaka yajadiliwe mambo
ambayo hayamo ndani ya rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba."
Chanzo:-Mtanzania Juni 11-2014
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment