Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Dunia inahesabu masaa kabla ya kuanza kushuhudia faina za kombe la dunia nchini Brazil huku kila timu ikijifua zaidi nchini humo huku usalama ukiwa umepigiwa msitari na jeshi la Brazil.
 
Ulinzi mkali wa jeshi unaousindikiza msafara wa timu hiyo popote uendapo uligeuka kero na kikwazo kwa wenyeji wa miji ya Brazili itakayoshuhudia mechi za fainali hizo zikichezwa.

Mjini Rio de Janeiro hali imekua ngumu kwa wakazi wa mji huo hususan inapofika wakati timu zinapokwenda katika viwanja vya kufanya mazoezi ya kujiandaa na michezo ya kombe la dunia itakayowakabili kuanzia siku ya Al-khamisi ya wiki hii.
 
Jana wakazi wa jiji hilo walilazimika kusubiri kwa dakika 15 wakiwa barabarani kwa ajili ya kupisha msafara wa timu ya taifa ya Uingereza ambayo imepangiwa kufanya mazoezi kwenye kambi ya jeshi katika eneo la Urca.

Kimbembe cha kusubiri kwa muda huyo wakiwa katika foleni kilisababishwa na mshambuliaji wa klabu ya Everton Ross Barkley, ambae almanusura aachwe hotolini baada ya kushindwa kwenda na muda wa kujiandaa kabla ya kuingia kwenye basi kwa ajili ya kwenda mazoezini.

Tayari wachezaji wenzake walikuwa wameshaingia kwenye basi na msafara ukataka kuanza lakini ikabainika Ross Barkley hayupo garini, hivyo iliwalazimu maafisa wa timu ya taifa ya Uingereza kuwaomba walinzi wa kambi yao kufanya subra ambayo ilisababisha foleni kubwa.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top