Mtangazaji wa maarufu wa runinga Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’ akiwa hoi hospitali akisumbuliwa na ugonjwa wa Athma.
Akichezesha taya na paparazi wetu, Penny alisema anamshukuru Mungu anaendelea vizuri kwani alikuwa na hali mbaya baada ya kubanwa na ugonjwa wa Athma kwa siku tatu nzima akiwa anasaidiwa kupumua na mashine ya oxygen.
Mtangazaji maarufu
wa runinga Bongo, Peniel Mungilwa ‘Penny’ akisaidiwa kupumua na mashine
ya oxygen baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Athma.
“Ukweli nilikuwa na hali mbaya huwa nasumbuliwa na Athma mara kwa
mara lakini naweza kubanwa kwa siku moja ila ya safari hii imekuja kwa
nguvu sana kwa sababu ilikuja na mafua makali jambo lililosababisha
nilazwe kwa siku tatu katika Hospitali ya AAR huku nikipumua kwa
kutumia mashine, kweli Mungu ni mkubwa, ninaendelea vizuri,” alisema
Penny.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment