Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kupokea
msaada wa hundi ya milioni kumi kutoka Zantel kwa ajili ya Chama cha
Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) leo jijini Dar es Salaaam, kushoto ni
Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose.
Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
(kulia), Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose (kushoto) pamoja na
viongozi kutoka Chama cha Ngumi Tanzania (BFT) wakiunganisha mikono
kwa pamoja kuonyesha ushirikiano wakati wa makabidhiano ya hundi ya
shilingi Milioni kumi kama msaada kutoka Zantel kwa Chama cha Ngumi
Tanzania (BFT).
Rais wa
Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Mutta Rwakatare akitoa shukrani kwa Zantel
baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi kuinua mchezo wa
ngumi, kushoto ni Katibu Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Makole Mashaga na
kulia ni Mjumbe wa Maendeleo ya Wanawake Bi. Aisha George
Voniatis. Picha na Genofeva Matemu.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment