Baadhi ya majirani wakishuhudia uokoaji wa ajali ya moto.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilomba, Amir Kitululu akizungumza jambo akiwa katika eneo la tukio.
Baadhi ya vitu vikiwa vimenusurika kutokana na ajali hiyo.
Mama mzazi wa Marehemu, Winfrida Sokon akiwa anashangaa bila kuamini kilichotokea baada ya moto kumwangamiza mwanaye.
MTOTO
mwenye umri wa miaka Mitatu na nusu aliyefahamika kwa jina la Rehema
Patrick amefariki dunia baada ya chumba alichokuwa amelala kuteketea kwa
moto.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kuongeza kuwa limetokea leo asaubuhi majira ya saa moja asubuhi
huko katika Mtaa na kata ya Ilomba jijini Mbeya.
Amesema
chanzo cha moto huo hakijafahamika ambapo mtoto huyo ambaye ni marehemu
alikuwa amelala wakati mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la
Winfrida Sokon (30), alikuwa ameenda kuchota maji huku naye baba yake
akiwa safarini.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti wa Mtaa, Amiri Kilulu, amesema Mama huyo ni mgeni
amehamia jana tu akiwa na watoto wawili ambao ni Tukulamba Mwakyami(4)
pamoja na marehemu, lakini huyo mkubwa ndiye aliyegundua moto huo.
Amesema
mtoto huyo baada ya kugundua moto huo alimfuata mama yake alikokuwa
akichota maji lakini walipofika walikuta mtoto ameshafariki dunia ambapo
majirani walijaribu kuuzima bila mafanikio.
Jeshi
la polisi lilifika eneo la tukio na kuondoka na marehemu kwa ajili ya
uchunguzi zaidi huku majirani nao wakichangishana fedha kwa ajili ya
kusaidia mazishi kutokana na ugeni wa mwanamke huyo.
NA MBEYA YETU
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment