Serikali ya Uturuki imeondoa marufuku ya miezi miwili iliyowekwa dhidi ya mtandao wa kijamii wa YouTube .
Hatua hii inakuja baada ya mahakama ya juu zaidi
nchini humo kuwaamuru maafisa wakuu kurejesha huduma za mtandao huo,
ikisema kuwa marufuku hiyo ilikiuka sheria za uhuru wa kujieleza.
Marufuku hiyo iliwekwa mwezi Machi , baada ya kanda kuhusu madai ya ufisadi nchini humo kusambazwa kwenye mtandao huo.
Uturuki ilipitisha sheria yenye utata mapema
mwaka huu ambayo iliwaruhusu wenye kutoa huduma hiyo kuikomesha bila
kufuata amri ya mahakama.
Maafisa wakuu waliendelea kubana YouTube hadi Jumanne licha ya uamuzi wa mahakama ukitoa wito kwa serikali kuondoa marufuku hiyo.
Uamuzi huo wa mahakama ya juu zaidi pia
unaonekana kama kupuuza serikali ya waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan,
ambayo imekuwa ikikosoa vikali mitandao ya kijamii.
YouTube imewahi kubanwa tena nchini Uturuki mwaka 2007, lakini marufuku hiyo iliondolewa mwaka 2010.
Chanzo bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment