Muigizaji nyota kutoka Kenya
Lupita Nyong'o amejumuishwa katika wasanii watakaoigiza katika filamu ya
Americanah inayotokana na kitabu cha mwandishi Chimamanda Ngozi
Adichie.
Muigizaji huyo aliwaambia mashabiki wake kuwa ni heshma kubwa kwake kupewa nafasi ya kuigiza katika filamu hiyo inayotokana na kitabu cha bi Adichie.
Kitabu hicho cha Americanah, kiachoelezea maisha ya wapenzi wawili Ifemelu na Obinze, chenyewe kinasifa si haba.
Kitabu hicho kilishinda tuzo la ''US National Book Critics Circle Award mwaka uliyopita.
Nyongo aliiambia BBC kuwa baada ya kukisoma kitabu hicho , alitamaushwa na jinsi Ifemelu na mpenzi wake Obinze,walivyostahimili majaribu mengi katika uhusiano wao .
Hali ambayo inawakumba waafrika wengi ambao kutokana na tamaa ya mafanikio wanakwenda ughaibuni kutafuta ajira na wengine kwa masomo ya juu.
Mbali na Americanah ,Adichie anajivunia tajriba ya uandishi wa vitabu vingine kama vile Purple Hibiscus na Half of a Yellow Sun,ambayo pia imefasiriwa na kuigwa katika filamu na muigizaji nyota katika 12 Years a Slave , Chiwetel Ejiofor.
Nyong'o aliwatamausha wapenzi wa filamu kote duniani aliposhirikiana na Ejiofor na kutwaa taji la Oscar katika 12 years a slave.
Nyongo vilevile amejiunga na wasanii katika filamu ya Star Wars.
<<BBC>>
BOFYA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment