Kijana
mmoja aliyejulikana kwa jina la Jumanne Joel(25-30) ameuawa na wananchi
wenye hasira kali baada ya kumvamia Monica Lutonja(32) wa kijiji cha Nyankumbu katika kata ya Kalangalala mjini Geita .
|
Bi.Monica Lutonja akiwa anauguza majeraha yake katika hospitali ya wilaya ya Geita jana baada ya kukatwa na mapangwa .Picha na Valence Robert- Malunde1 blog-Geita.
|
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo inadaiwa kuwa watu watatu
akiwemo marehemu walienda kwa mama huyo na kugonga hodi wakidai kuwa wao
na rafiki wa kaka yake ambaye ni Bunegezi.
Baada ya Monica Lutonja kufungua walianza kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kupoteza fahamu.
Hata
hivyo kelele za mama huyo zilisababisha majirani kutoka na kuanza
kuwasaka baada ya kuwa wamekimbia na hatimaye wakamkamata mmoja na
wakaanza kumpiga hadi kumuua.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibisha kutokea kwa tukio hilo
na kuongeza kuwa watuhumiwa wengine wawili bado wanatafutwa na jeshi
la polisi kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Na Valence Robert-Malunde1 Blog- Geita
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment