Shimo ambamo kichanga hicho kimekutwa
Mashuhuda wakishuhudia
Wengine wakiwa wameduaa
Watoto wakiwa wanatimuliwa eneo la tukio
****
WIMBI
la wanawake mkoani Mbeya kujifungua watoto na kisha kuwatupa na wengine
kutoa mimba limezidi kushika kasi na kukithiri baada ya vitendo hivyo
kuripotiwa na vichanga kuokotwa kwenye mashimo na mitoni.
Kukithiri
kwa vitendo ni baada ya leo Wananchi wa Mtaa wa Mwambenja kata ya
Iganzo jijini Mbeya kugundua kutupwa kwa mtoto anayesemekana kuwa na
umri usiozidi siku moja jinsia ya kike katika shimo la choo
kisichotumika.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti wa Mtaa huo, aliyefahamika kwa jina la Lukasi
Mwakalonge, alisema alipewa taarifa na wananchi wake mchana na kuambiwa
kuna katoto kametupwa shimoni na bado ni kazima hali iliyomlazimu kutoa
taarifa katika Jeshi la Polisi.
Alisema
baada ya kufika eneo la tukio na kugundua kuwa mtoto bado yuko hai
wakaamua kumtoa ndani ya shimo huku wakisubiri jeshi la polisi kwa ajili
ya hatua zaidi lakini akawa amepoteza maisha muda mfupi baada ya
kutolewa ndani ya shimo.
Hata
hivyo jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa
marehemu, vitendo hivyo vya wanawake kutupa watoto kabla na baada ya
kujifungia bado vinazidi kutokea hapa nchini ingawa hakuna takwimu
sahihi za wanawake waliopatikana na hatia kwa makosa kama hayo.
NA MBEYA YETU
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment