Wapiganaji
wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram wamewateka nyara wanawake 20
kutoka jamii inayohamahama Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Wanawake
hao walichukuliwa katika Makazi ya Gakini Fulani karibu na mji wa
Chibok ambako zaidi ya wasichana wanafunzi 200 walitekwa nyara Aprili,
mwaka huu.
Walioshuhudia
tukio hilo walisema kuwa wapiganaji hao waliokuwa wamejihami kwa
bunduki waliwalazimisha wanawake hao kuingia katika magari yao kabla ya
kutoroka nao katika Jimbo la Borno.
Mlinzi
mmoja wa kijiji alisema kuwa washambulizi hao pia waliwateka nyara
wanaume watatu waliojaribu kuwazuia wasiondoke na wanawake hao. Hadi
sasa jeshi halijasema lo lote kuhusiana na tukio hilo.
Katika
hatua nyingine, jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua wapiganaji 50
katika kampeni yake dhidi ya magaidi mwishoni mwa wiki katika majimbo
ya Borno na Aladawa.
Mfululizo wa mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo umeimarisha ukosoaji wa vyombo vya usalama vya Serikali.
Licha
ya kuwepo kwa hali ya hatari katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa
Nigeria wanajeshi hawajachukua hatua thabiti kukabiliana na hali
hiyo.
Chanzo: BBC
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment