U.T.I kirefu
chake ni Urinary Tract Infection ni maambukizi ya bakteria mbalimbali
wanaoshambulia mfumo wa mkojo, yaani kwenye figo (kidney), kibofu cha
mkojo na mifereji inayotoa mkojo (urethra)
Mifereji
inayotoa mkojo kwenye figo (ureter) na mfereji unaotoa mkojo nje, mara
nyingi bakteria hushambulia sehemu za chini za mfumo wa mkojo yaani
urinary bladder na kitaalamu kuitwa bladder infection.
Bakteria
hao baada ya kumuingia binadamu hupona mara moja pindi mgonjwa
anapoanza dozi lakini kama wadudu hawa hawatatibiwa vizuri wanaweza
kupanda na kushambulia figo na mshipa unaounga sehemu hiyo uitwao renal
pelvis na kuleta madhara makubwa, hivyo kusababisha ugonjwa wa figo.
Kuna
wadudu wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wa binadamu ambao kila binadamu
anaishi nao, hawa husaidia kulinda mwili na kitaalamu hujulikana kama
normal flora na huwa ni askari wa mwili.
Vijidudu
hivyo hushuka hadi kwenye mlango wa haja kubwa na kuenea mpaka sehemu
za siri. Kama wataingia kwenye mfumo wa mkojo hushambulia sehemu hizo
kwani wadudu hao wanakuwa hawajazoea mazingira ya sehemu za mkojo.
WANAWAKE WANAVYOSHAMBULIWA NA UTI
Mara nyingi wanawake ndiyo wanaoshambuliwa kirahisi na bakteria wa UTI kutokana na maumbile yao ya sehemu za siri.
Sababu kubwa ya kushambuliwa kirahisi ni kwa kuwa wanakuwa na mfereji mfupi wa kutoa nje mkojo (shot urethra).
Sababu nyingine inayosababisha UTI ni kutokumywa maji kwa wingi, hivyo kushindwa kwenda haja ndogo mara kwa mara.
Kama mtu
ana ugonjwa wa mawe kwenye figo (kidney stone) pia kwa wanaume wenye
ugonjwa wa kuvimba tezi la manii (enlarged prostate), wana uwezekano wa
kukumbwa na maradhi haya.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment