
Mamake Farzana akiomboleza kifo cha mwanawe
Mwanamke mmoja nchini Pakistan
amepigwa mawe na familia yake wakiwemo babake na ndugu zake wa kiume
hadi kufariki. Aliuawa nje ya jengo la mahakama mjini Lahore.
Mwanamke huyo aliuawa kwa kuolewa na mtu ambaye alikuwa chaguo lake mwenyewe.
Farzana Bibi, mwenye umri wa miaka 31, aliolewa na Muhammad Iqbal miezi michache iliyopita bila ya idhini ya familia yake.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alishambuliwa na familia yake.
Kaka zake na binamu yake mmoja walimshika alipokuwa akiingia mahakamani na kuanza kumpigwa kwa mawe . Alifariki popo hapo.
Waliomuua walikimbia kabla ya polisi kufika katika eneo hilo.
Babake msichana huyo amekamatwa ingawa washukiwa wengine wangali hawajulikani waliko.
Kwa wanawake wanaoolewa na wapenzi ambao ni
chaguo lao wenyewe, ni kitendo kisichokubalika kitamaduni katika baadhi
ya maeneo ya Pakistan.
Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu,
wanaamini kuwa kwa kuwa mauaji hayo hufanywa na familia zenyewe, huwa ni
vigumu kufikisha kesi hizo kortini.
>>>>Chanzo bbc
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment