Ndugu yangu msomaji wa habari hii, kwanza nakuomba unisamehe kwa kupost picha hii yenye kutisha, lakini sikuwa na jinsi ya kufanya imenibidi nikaiweke ili ujionee tukio zima lilivyokuwa.
Tukio
hili la kusikitisha limetokea kwenye maeneo ya Buzuruga ambapo kijana
mmoja ambaye alikuwa amebebwa katika pikipiki amejikuta akipoteza maisha
yake baada ya zile haraka haraka za dereva wa bodaboda kutaka kuwahi
ikabidi dreva huyo mwendesha bodaboda avunje sheria za usalama
barabarani.
Baada ya
kuvunja sheria ndipo alijikuta akiovateki roli kubwa ambalo mteja wake
huyo alijikuta akinasa kwenye roli hilo ubavuni, sababu ya kunasa kwenye
roli hilo nikutokana na kwamba kijana huyo alikuwa amebeba kibegi
kidogo mgongoni mwake ambacho kilikuwa ndicho chanzo cha kunasa kwake.
Kijana
huyo alijikuta akiingia kwenye uvungu wa roli hilo na ndipo dimbwi la
damu pamoja na umauti ukawa umemfika pale pale alipokuwa.
kiukweli
kijana huyo hakuweza ata kuomba maji ya kunywa zaidi ya roho yake
kutoweka na huku akiacha damu ikitapakaa kama maji kwenye eneo la tukio.
Kiroho
tupo nae lakini kimwili hatutomuona tena kijana huyu, sikubahatika
kulijua jina lake mapema ila kwakuwa sote ni binadamu na wote ni ndugu
hatuna budi basi kumuombea afike salama uko aendako.
tumuombee ili aweze kupokelewa vyema mbele ya Mungu wake, Mungu ailaze roho ya marehemu milele maari pema peponi
CHANZO MTALEMWA BLOG
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment