
Kwenye
zile stori za maisha ya mastaa wa soka Ulaya wiki hii, hii nayo ni moja
ya stori kubwa ambapo ilisambaa kupitia vyombo mbalimbali vya habari
likiwemo gazeti la Daily Mail lililoripoti kuhusu gari la mchezaji huyu
wa Manchester City kubebwa juujuu na Polisi kwa makosa ya kupaki ovyo.
Ripoti
ilitoka kwamba staa huyu ambae atalitazamia kombe la dunia nyumbani kwa
sababu hajapangwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa amepata
habari nyingine isiyo nzuri baada ya gari lake kubebwa juujuu kutokana
na makosa ya parking, yani liliegeshwa kimakosa.
Pamoja
na kwamba ripoti ilisema Samir atalazimika kwenda kulichukua hili gari
yeye mwenyewe kwenye mamlaka husika, staa huyu alikanusha kuwa mmiliki
wa hilo gari na kusisitiza kwa kuliambia gazeti ‘Daily mail fanyeni
utafiti, hilo halijawahi kuwa gari langu’

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment