Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi kwenye Viwanja vya Kibanda Maiti, mjini Zanzibar, Mei 4, 2014 kueleza kwa nini CCM inawataka Watanzania kuiunga mkono kuhusu msimamo wake wa kutaka Tanzania iendelee kuwa katika mfumo wa serikali mbili ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar baada ya mchakato wa Katiba mpya.
Mjane wa Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, Mama Fatuma Karume akizungumza kwenye mkutano huo.
 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshukuru na kumpongeza Mama Fatuma Katume kwa hotuba nzuri 'iliyoshiba'.
Ni serikali mbili tu:  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, akionyesha alama inayotumiwa na chama chake kujinasibu kuwa kinahitaji serikali mbili katika katiba mpya, alipohutubia wananchi katika mkutano huo wa Kibanda maiti, Mei 4, 2014 mjini Zanzibar.
Kada machacahari wa CCM kutoka Zanzibar, Asha Bakari Machano akihutubia mkutano huo wa Kibanda maiti, Mei 4, 2014.
Kada mwingine ambaye pia ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alitema cheche kwenye mkutano huo, wakati akieleza kwa nini CCM inaona kwamba mfumo wa serikali mbili  katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo unafaa.
Wananchi wakishangilia huku wakionyesha kuunga mkono msimamo wa CCM wa kutaka mfumo wa serikali mbili katika katiba mpya, wakati wa mkutano huo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top