WATU wasiozidi 50 wamenusurika kifo baada ya
basi dogo kupinduka katika eneo la Sinai nje
kidogo ya mji wa Songea mkoani Ruvuma kutokana
na uzembe wa abiria .Ajali hiyo ilisababisha na
mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni askari wa
jeshi la kujenga Taifa JKT Mlale Songea ambaye
alikuwa ni mmoja wa abiria kuamua kuendesha
basi hilo baada ya dereva wa basi kutelemka na
kumsaidia dereva mwenzake ambaye basi lake
lilikuwa limeharibika.Dereva wa basi lililopata ajali
Bernad Bernad maarufu kwa jina la Kichefuchefu
alisema yeye baada ya kutelemka kwenda
kumsaidia dereva mwenzake alishangaa kuona gari
lake linarudi nyuma likiendesha na mmoja wa
abiria kisha kupinduka baada ya abiria huyo
anayedaiwa kuwa ni mwanajeshi kushindwa
kulimudu kuendesha .Bernad alisema kuwa mabasi
madogo matatu yalikodiwa na familia za askari wa
jeshi la kujenga Taifa Mlale ili kufika mjini Songea
na kwamba wakiwa katika eneo la Sinai ndipo basi
moja lilikuwa na hitilafu ndipo mabasi yote
yalisimama ili kwenda kumsaidia mwenzao ili
waweze kuendelea na safari ya mjini Songea.
“ Baada ya kutelemka nilishangaa kuona gari
yangu inarudi nyuma kwa kasi kisha ikaanguka
ikiwa na abiria ambao walipata majeraha na
kukimbizwa katika hospitali ya Peramiho,mtu
aliyesababisha ajali anayedaiwa kuwa ni askari wa
JKT Mlale mara baada ya ajali amekimbia msituni
tulijaribu kumkimbiza tumeshindwa
kumkamata’’,alisema Bernad.
Hata hivyo mwandishi wakati anapita katika eneo
la ajali hakuweza kukuta mtu yeyote aliyekuwepo
kwenye ajali hiyo zaidi ya dereva wa basi
hilo,utingo na wapita njia ambao walitoa lawama
kwa askari huyo aliyeamua kuendesha gari wakati
yeye alikuwa ni abiria na kusababisha ajali kwa
uzembe.
Credit: Kwanzajamii.
Ajali mbaya yatokea ikisababishwa na Abiria aliepindua basi. Fahamu kilichotokea
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment