Ugonjwa wa maumivu katika magoti au kiuno kitaalamu huitwa Osteoarthritis.
Ugonjwa huu huwapata watu wengi hasa wenye unene wa kupita kiasi au wazee. Osteoarthritis ina maana magonjwa ya viungo vya mwili kiujumla, lakini hasa hushambulia magoti na kiuno.Ni ugonjwa wa muda mrefu na kusababisha uharibifu wa minofu migumu myeupe katika magoti, au kitaalamu huitwa cartilage articular.
Ugonjwa huu umekuwa wa kawaida kwa watu wengi, lakini katika nchi yetu ni vigumu kusema ni kiasi gani watu wanaathirika.
Lakini njia rahisi ya kuugundua ni
kupiga x-ray. Sababu kubwa za ugonjwa huu ni uzee, magonjwa ya kurithi,
matokeo ya majeraha ya zamani katika magoti, mabadiliko ya homoni za
estrojen, unene, udhaifu wa misuli na uchovu uliokithiri hasa kwa
wanamichezo, kazi ngumu, hasa za kusimama au kunyanyua vitu vizito.nk na
michezo ya kawaida.
DALILI
Wengi hupenda kuangalia dalili kwani matokeo ya x-ray hayatoshelezi kinaganaga. Mtu aliyepatwa na ugonjwa huu atasikia maumivu makali yatokanayo na kuzidiwa kwa uzito katika magoti.
Wengi hupenda kuangalia dalili kwani matokeo ya x-ray hayatoshelezi kinaganaga. Mtu aliyepatwa na ugonjwa huu atasikia maumivu makali yatokanayo na kuzidiwa kwa uzito katika magoti.
Maumivu hayo atayapata wakati wa
kusimama au kutembea, hizi ndizo dalili za kwanza. Hali hii hutokana na
kupungua kwa misuli myeupe iliyopo katika goti na kufanya nafasi au
mwanya kati ya goti kupungua au hata kuwa inasuguana hivyo kusababisha
maumivu makali.
TIBA
Kwa sasa hakuna tiba kwa ajili ya Osteoarthritis, lakini njia kadhaa za kupunguza dalili na kuchelewesha mchakato wa kuendelea kukua kwa ugonjwa huu zaweza tumika.
Hapo awali watu walitumia madawa ya kupunguza maumivu, lakini leo hii tiba ya msingi ni kufanya mazoezi ya kupunguza uzito.

Hii ni kwa kuwa imeonekana njia hii
hufanya kazi vizuri zaidi kuliko kutumia vidonge vya kupunguza maumivu,
ambavyo wengi huwaletea matatizo ya tumbo kama vile vidonda vya tumbo
n.k.
Mazoezi hupunguza maumivu kwa mgonjwa na kuongeza ubora wa maisha katika osteoarthritis na uzuri ni kuwa hakuna athari kwa kufanya mazoezi.
Mazoezi hupunguza maumivu kwa mgonjwa na kuongeza ubora wa maisha katika osteoarthritis na uzuri ni kuwa hakuna athari kwa kufanya mazoezi.
Mazoezi hayapaswi kuchanganywa na
aina yoyote ya shughuli za kimwili, isipokuwa mazoezi ni vizuri yawe ya
kulenga uimara wa viungo vya mwili hasa katika magoti.
Na vizuri yasiwe ya nguvu kiasi cha kukufanya ukaumia zaidi.
USHAURI
Inashauriwa kuwa mazoezi hayo yafanyike kwa muda wa wiki sita hadi kumi .
Inashauriwa kuwa mazoezi hayo yafanyike kwa muda wa wiki sita hadi kumi .
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment