
Mahakama moja nchini Misri
imewahukumu watu wanne kifungo cha hadi miaka minane jela kwa kosa la
vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Hukumu hiyo imeshutumiwa na wanaharakati wa haki za binadamu.
Mmoja wa watu hao amehukumiwa na mahakama mjini Cairo, kifungo cha miaka mitatu jela na kazi ngumu.
Kikundi cha kutetea haki za binadamu chenye
makao yake nchini Marekani, Human Rights First , kimesema hukumu hizo
zinasikitisha na kukatisha tamaa.
"Misri ni taifa linalobadilika katika eneo la
nchi za Kiarabu; kinachotokea Misri kinaweka hali ya kuenea katika
ulimwengu wote wa nchi za Kiarabu," kimesema kikundi hicho katika
taarifa yake.
Kikundi hicho kimesema tangu kung'olewa
madarakani Rais Mohammed Morsi mwezi Julai 2013 kumekuwa na ongezeko la
watu kukamatwa kwa misingi ya jinsia zao.Hukumu ya sasa inakumbushia kesi ya mwaka 2001 ya watu 52 kushutumiwa kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na makosa mengine chini ya sheria ya Misri.
Watu ishirini na watatu walihukumiwa kifungo cha kufikia miaka mitano jela pamoja na kazi ngumu, hukumu ambayo ilishutumiwa kimataifa.
>>>>>Chanzo bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment