
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho
Meneja wa timu ya Chelsea ya
Uingereza Jose Mourinho ametozwa faini ya pauni £8,000 na ameonywa
kuhusu mwenendo wake baada ya kutolewa nje katika mechi ya mwezi
uliopita pale Chelsea ilipokubali kipigo cha Aston Villa cha goli1-0.
"Sijui ni kwa nini nilitolewa nje ," Mourinho alihoji baada ya mchezo.
"Niliuliza, lakini mwamuzi alikataa kuzungumza nami."
Mourinho alimshutumu Foy ada ya mchezo katika
uwanja wa Villa Park katika matokeo ambayo yalisababisha Chelsea
iliyokuwa ikiongoza ligi kuu ya England kupoteza pointi nne.
Ramires alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa
moja kutokana na kumchezea vibaya mchezaji wa Aston Villa, Karim El
Ahmadi, kitendo kilichosababisha vurugu kiasi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment