
Umoja wa
mataifa Nchini Sudan Kusini umejitetea vikali kutokana na ukosoaji
kwamba inawabagua watu wanaotaabika ndani ya makao yake makuu katika
jiji kuu la Sudan Kusini Juba.
Wakimbizi
hao wamekita kambi kwenye ofisi za umoja wa mataifa baada ya kukimbia
mapigano kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kirr Mayardit na
aliyekuwa makamu wake Riek Machar.
Mnamo jumatano wiki hii, kundi la
madkatari wasio na mipaka Medecins Sans Frontieres lilisema kuwa watu
elfu 20 wanaishi katika hali ya mateso makubwa baada ya mvua iliyonyesha
majuzi na kusababisha vyoo kufurika nakuporomoka
.Toby Lanzer, naibu mkuu wa umoja wa
mataifa mjini Juba ameiambia BBC kuwa wanatamaushwa pia na hali mbaya ya
maisha ya watu hao waliokimbia mapigano.Lakini amesema kuwa kambi hiyo
ya muda haikuwa ihudumie idadi kubwa ya watu.
Aidha amesema kuwa wanafanya kila
wawezalo ili kuboresha sehemu hiyo mbali na kujaribu kukodisha shamba
lililo maeneo ya nyanda za juu viungani mwa mji mkuu ili kujenga kambi
nyingine ya muda ya kuwahudumia watu.

Shirika moja lisilo la kiserikali la
madaktari wayo na mipaka , Medecins Sans Frontieres (MSF) lilitoa picha
na habari zilizosimulia hali mbaya wanayostahimili wakimbizi wa ndani
kwa ndni nchini Sudan Kusini huku Wafanyikazi wa shirika la umoja wa
mataifa linalosimamia maswala Sudan UNMISS likipuzilia mbali masaibu
yao.
MSF ilitoa picha ya Kambi hiyo ambayo
inawatu takriban 21,000 wakiishi katika kambi ambayo maji taka
yamezagaa kwote .Shirika hilo lilitoaushahidi kuwa vyoo 150 vya kambi
hiyo vimeporoka na uchafu umetapakaa ovyo.
Zaidi ya watu milioni moja wametoroka
makwao .Takriban watu , 803,200 ni wakimbizi wa ndani kwa ndani huku
wengine 254,000 wametoroka nchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment