Kufuatia
taarifa hizo, tayari uchunguzi umeanza kuhusu eneo ambako sauti hizo
zilibainika ingawa ni sehemu tofauti kabisa na ile ya awali ambayo
ilionekana kwenye picha za Sattelite za nchi ya Australia na China.
Kitengo
maalumu kinachoratibu zoezi la utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo,
kimesema kuwa licha ya dalili nzuri za kubaini sauti hizi, bado
hawajapata uhakika wa asilimia mia moja iwapo kile kilichogundulika
huenda kikawa ni kisanduku cheusi cha mawasilaino ya ndege hiyo.
Mkuu
wa operesheni za Australia kwenye utafutaji wa ndege hiyo, Angus
Houston, amesema taarifa hizi zilizotolewa sasa zinaendelea kuchunguzwa
kwa umakini mkubwa.
Iwapo
kisanduku hicho cha sauti hakitapatikana ndani ya siku mbili zijazo
huenda ikawa ngumu zaidi kukipata kwa siku zijazo kwa kuwa siku 30
zimetimia kwa kisanduku hicho kupoteza nguvu yake.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment