![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/04/11/140411165100_nyumba_ginday_512x288_bbc_nocredit.jpg)
Nyumba walimokuwa wanaishi Ginday na marehemu mkewe
Mwanamume mmoja aliyekuwa mfanyakazi wa benki nchini Uingereza, amefungwa maisha jela kwa kumuua mke wake.
Jasvir Ginday aliambia mahakama kuwa alimuua
mkewe baada ya kumtishia kuwa angewaambia wazazi wao kuwa mume wake
hushiriki mapenzi ya jinsia moja.
Mahakama ilisikia Ginday alivyomnyonga mkewe na kisha kuchoma mwili wake.
![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/04/11/140411164615_ginday_wife_304x171_bbc_nocredit.jpg)
Harusi ya wawili hao ilikuwa harusi ya kupangwa
Kesi hii ilisikikilizwa kwa wiki tatu.
Lakini alikuwa amemwambia rafiki yake mwaka 2008 kuwa yeye huvutiwa zaidi na wanaume licha ya kwamba alikuwa anamuoa mchumba wake Varkha aliyekuwa na miaka 24.
![](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/04/11/140411164742_ginday_person_304x171_bbc_nocredit.jpg)
Jasvir Ginday
Wakati kesi ilipokuwa ikiendelea, Ginday alidai
kuwa mkewe alitishia kufichua kwa familia zao kuwa aliozwa mwanamume
ambaye hushiriki mapenzi ya jinsia moja baada ya kupata picha chafu
kwenye simu yake.
Aliambia mahakama kuwa baada ya mkewe kupata
picha hizo alikimbia chumbani na kumtishia na hapo ndipo alipomgonga na
chuma kichwani na kumuua kutokana na hasira.
>>>>Chanzo bbcswaili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment