Mjadala umezuka nchini Rwanda ambapo baadhi
ya wananchi wanataka kurejeshwa kwa hukumu
ya kifo nchini kufuatia kesi dhidi ya mwanamme
mmoja, mtumishi wa nyumbani, anayetuhumiwa
kumuua mtoto wa kike kwa kumkata kichwa.
Rwanda haina hukumu ya kifo na baadhi ya
wananchi wameelezea haja ya
serikali kufanya marekebisho ya sheria ili
kuirejesha hukumu hiyo.
Kesi dhidi ya mwanamume huyo awali iliendeshwa
hadharani katika uwanja wa mpira mjini Kigali na
polisi walikuwa na wakati mgumu kumlinda dhidi
ya watu waliokuwa na hasira waliotaka auwawe.
Mamia ya watu walijitokeza kwenye uwanja wa
michezo wa Nyamirambo kushuhudia kesi
iliyofanywa hadharani kwa mara ya kwanza.
Mamia ya watu walijitokeza kusikiliza kesi
inayomkabiliwa Sylivester Hola, ambaye alimuua
msichana mwenye umri wa miaka 12, aliyekuwa
binti wa mwajiri wake, ambaye amemfanyia kazi
zaidi ya miaka 10.
Maafisa wa polisi walikuwa na muda mgumu
kujaribu kuwazuia watu waliotaka kumwadhibu
mtu huyo wenyewe.
Raia mmoja wa Rwanda, ambaye hakutaka jina
lake kutajwa aliiambia BBC kuwa hukumu ya kifo
ni sharti irejeshwe:
"mtu anayeua kwa kisu anapaswa kuuawa kwa
risasi au apigwe risasi na auwawe ili uwe mfano
kwa watu wengine kama yeye," mtu huyo alisema.
CHANZO: BBC SWAHILI
MJADALA KUHUSU HUKUMU YA KIFO WAZUKA NCHINI RWANDA.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment