Watu zaidi ya 20 wamepoteza maisha na wengine
kujeruhiwa vibaya wilayani Busega Mkoani Simiyu
leo asubuhi kufuatia ajali ya Bus la kampuni ya
Luhuye iliyopasuka mpira, kuacha njia na
kugonga nyumba.
Mbunge wa Jimbo la Busega ambaye pia ni Waziri
wa uvuvi na maendeleo ya Mifugo Dakta Titus
Kamani ameiambia Blog hii kwa njia ya Simu
kwamba ajali hiyo imetokea katika kijiji cha
Sogesita wilayani humo.
Dakta Kamani amesema basi hilo lilikuwa
likielekea Jijini Mwanza ndipo lilipopasua mpira
wa mbele na kupinduka huku likigeukia lilikotoka
kabla ya kuacha njia na kugonga nyumba kwenye
kaya moja kijijini hapo.
Amesema, idadi kamili ya waliopoteza maisha na
hali za majeruhi itafahamika baadaye
Chanzo:farajimfinanga.com
WATU ZAIDI YA 20 WAFARIKI PAPO HAPO BAADA YA BASI KUGONGA NYUMBA NA KUPINDUKA MKOANI SIMIYU
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment