Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Wiki hii
mitandao ya
Nigeria
iliripoti kuwa
kulikuwa na
ugomvi
mkubwa kati
ya mapacha
wanaounda
kundi la
PSquare, Peter na Paul Okoye na kwamba
walitaka kupigana wakati wakiwa mazoezini.
Habari hizo zilichochewa na tweet ya kaka yao
mkubwa ambaye ni meneja wao, Jude Okoye
iliyootafsiriwa na mitandao hiyo kuwa huenda
ameachana na kundi hilo baada ya kuwepo
ugomvi kati yake na ndugu hao kutokana na
msimamo wake wa kutohudhuria ndoa ya
kisasa ya mdogo wake itakayofanyika Dubai.
Mitandao hiyo iliandika kuwa Jude Okoye
hapatani kabisa na mke wa Peter Okoye, Lola
Omotayo.
“After over 10 years of hard work, it’s over.
Am done.” Alitweet Jude Okoye.
Hata hivyo, msemaji wa kundi hilo
anaejulikana kama Bayo Adetu amekanusha
habari hizo wakati akiongea na Premium
Times na kudai kuwa hafahamu habari hizo
zimetoka wapi.
“I am too busy to give some wanna be
blogger traffic, I don’t know where that report
is coming from. Maybe they just want to get
traffic to their site. It’s baseless and untrue.”
Amesema Bayo Adetu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top