
Utetezi wa
muundo wa Muungano wa serikali mbili katika mjadala wa katiba jana
ulichukua sura mpya kwa kuelekeza mashambulizi mengi dhidi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa ni mtu
kigeugeua sawa na kinyonga.
Mashambulizi
hayo yalianza asubuhi wakati Mohammed Seif Khatib alijadili sura ya
kwanza na ya sita ya rasimu ya katiba, akimwelezea Maalim Seif kuwa ni
mtu anayebadilika kama kinyonga, kiasi cha kudirikia kuiba nyaraka Ikulu
iliku kuulinda Muungano wa serikali mbili, lakini sasa amegeuka na
kusaka serikali tatu na Muungano wa mkataba. Khatib alisema kuwa Maalim
Seif aliwachongea viongozi wa Zanzibar, akiwamo Rais wa awamu ya pili,
Abood Jumbe, ili kutetea Muungano wa serikali mbili.
Mbali na
Jumbe, wengine wanaodaiwa kuchongewa na Maalim Seif mwaka 1984, ni
Waziri Kiongozi mstaafu, Ramadhani Haji Fakhi, na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Wolfgang Dourado, wa wakati huo. Alisema Maalim Seif
aliwashitaki viongozi hao kwa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius
Nyerere na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano wa
Kamati Kuu (CC) ya chama hicho mwaka huo akidai kwamba walitaka
kubadilisha katiba na kuwa na Muungano wa serikali tatu.
Khatib
alisema Maalim Seif alidai kuwa Dourado alikuwa anasafiri kati ya London
na Zanzibar ili kukashifu viongozi wa Muungano na kuwachochea watu
wauchukie kuwa siyo wa halali. Alisema Maalim Seif alidai kuwa kwa
safari hizo Dourado aliangamiza fedha za kigeni na kuhoji alipata wapi
jeuri ya kuwasemea Wazanzibari. Khatib alimnukuu Maalim Seif akisema
kuwa viongozi hao walifanya vitendo vya uhaini na kutaka Halmashauri Kuu
(Nec) iwahukumu.
Alinukuu
kauli za Maalim Seif aliyesema: “Suala la serikali tatu limepewa uzito
mkubwa katika waraka na linachochewa na Makamu Jumbe.” Aidha, alimtuhumu
Maalim Seif kuwa ni kiongozi wa ajabu aliyediriki kuiba waraka wa siri
kwenye Ikulu ya Zanzibar na kuungama kuwa alifanya hivyo kama
alivyonukuliwa kwenye kitabu cha Profesa Issa Shivji. Khatib alisema
Maalim Seif aliiba waraka huo kwenye shubaka (droo) ya Rais Ikulu ili
kutetea muundo wa serikali mbili. Alimfananisha Maalim Seif na kinyonga,
ambaye mwaka 1984 alitetea serikali mbili baada ya kutimuliwa CCM Mei
13, 1988, alitaka serikali tatu na mwaka jana akaibuka na Muungano wa
mkataba.
DK. MWAKYEMBE AONGEZA MASHAMBULIZI
Dk. Harrison
Mwakyembe naye aliendeleza mashambulizi dhidi ya Maalim Seif
alipomkariri katika moja ya hotuba zake akisema: “Naamini maslahi ya
Zanzibar yana uhakika zaidi katika Muungano huu, ambao umesaidia kuzuia
machafuko na kuepusha vifo vya watu wasio na hatia Zanzibar na kwamba,
ndiyo uliodumisha amani.” Alimnukuu akiahidi: “Nitaandelea kudumisha
Muungano na kuyatetea maslahi ya Zanzibar.”
Dk.
Mwakyembe alisema Maalim Seif licha ya kuteta serikali mbili katika
mfumo wa Muungano, aliwahi kudai kuwa kero zilizoko siyo za msingi. Naye
Hamad Rashid Mohammed alitumia fursa ya jana kuweka wazi walivyohusika
yeye na Maalim Seif kupeleka waraka wa Jume kwa Mwalimu Nyerere baada ya
kuongea na Waziri Mkuu, Edward Sokoine.
Hamad
alisema kuwa walimfuata Mwalimu Butiama baada ya kusoma waraka wa Jumbe,
aliitisha kikao cha Kamati Kuu lakini mwafaka haukupatikana ikabidi Nec
iitishwe na mwishowe maamuzi ya kuvuliwa madaraka Jumbe yalifikiwa.
Alisema kuwa Ali Hassan Mwinyi aliagizwa kugombea urais Zanzibar na
alitakiwa amteue Maalim Seif kuwa Waziri Kiongozi.
Alimshutumua
Maalim Seif kwa usaliti na kwamba anajitwisha Uzanzibari kuliko
Wazanzibari wengine, lakini kinachomsumbua ni kutaka madaraka tu kwani
alimfaia vitimbi pia Mzee Abdul Wakili, ambaye akiteuliwa kugombea urais
baada ya Mwinyi kuwa Rais wa Tanzania.
CHANZO: NIPASHE
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment