Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia Jiji la Mbeya Lucas Mwampiki amejiuzuru wadhifa huo kuanzia Aprili mwaka huu kutokana na mkanganyiko wa uongozi ndani ya chama hicho.


Mwampiki amesema amechoshwa na marumbano ya mara kwa mara na meza kuu ndani ya chama hicho katika ngazi ya wilaya hivyo kudhoofisha juhudi zake za kukijenga chama hicho.
Aidha Mwampiki amesema viongozi wa chama hicho wamekuwa na marumbano ya mara kwa mara hivyo yeye kama kiongozi hayupo tayari kuona mambo yanavurugika katika chama hicho.

Hata hivyo katika uamuzi aliouchukua Lucas Mwapiki amesema kuwa yeye atabakia kuwa mwanachama wa chama hicho na Diwani wa Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya.

Amewataka wanachama wamuelewe hivyo ameona yeye akae pembeni badala ya kuwa na muda mwingi wa kujadili migogoro ambayo haina tija na kuleta mkanganyiko kwa wanachama.

Na Ezekiel Kamanga
Mbeya

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top