
Rais Uhuru Kenyatta
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imehairisha kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta hadi tarehe saba Oktoba mwaka huu.
Mahakama kuu ya ICC, kupitia
mwendesha mashitaka Fatou Bensouda, imekuwa ikiitaka serikali ya Kenya
kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuendesha kesi zinazowakabili Rais
Kenyatta na naibu wake bwana Ruto.
Hii ni mojawapo ya sababu kuu ya kubadili tarehe ya kusikizwa kwa kesi hii.
Upande wa mashitaka umesema kuwa unaipa Kenya muda wa ziada ili kutafuta na kuwasilisha baadhi ya stakabadhi za benki zinazohitajika katika kesi hiyo.
Kumekuwa na malalamishi kutoka kwa upande wa mashitaka kuwa serikali ya Kenya inalenga kuzuia stakabadhi hizo kufikishwa mahakamani jambo ambalo mawakili wa bwana Kenyatta wamekanusha.
Miongoni mwa yale yanayohitajika kotini ni pamoja na taarifa ya maelezo ya fedha anazomiliki bwana Kenyatta.
>>>>>>Chanzo bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment