STAA wa filamu Bongo, Kulwa
Kikumba ‘Dude’ amewatoa nishai viongozi wa Bongo Muvi kwa kueleza kuwa,
risala iliyosomwa siku ya ‘bethidei’ yao ya kutimiza miaka mitatu
imepotosha ukweli.
Akizungumza na Ijumaa hivi
karibuni, Dude alisema ameshangaa kusikia kwenye risala hiyo kuwa
waanzilishi wa umoja huo ni Kanumba, Sajuki, Jimmy Mafufu na wengineo
wakati ukweli hauko hivyo.
“Ile risala imepotosha, Bongo
Muvi ilianzishwa na wasanii wa muziki na filamu wakiwemo mimi, William
Mtitu, H.Baba, Simon Mwakifwamba, MwanaFA na Fid Q na wengineo kwa
lengo maalum, nimeshangaa kusikia vile,” alisema Dude huku akisisitiza
kuwa, yeye hajisifii ila ukweli usipindishwe.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment