
Tamaa ya mchuzi wa nyama ya binadamu yatongea kaka wawili.
Ni visa mbavyo wengi tulivisikia
katika hadithi za kale, watu kuliwa na majitu, lakini katika siku za
karibuni tumeshuhudia watu wakila viungo vya wenzao Jamhuri ya Afrika ya
Kati katika jazba ya kulipiza kisasi dhidi ya watu waliowadhulumu
katika uongozi uliong'olewa mamlakani wa Seleka .
Hata hivyo wawili hao wameonekana kuwa na tamaa kubwa ya mchuzi wa nyama ya binadamu.Wakaazi hao wa kijiji cha Daryabn Khan jimbo la Punjab walikamatwa mwaka 2011.
Polisi walisema kwamba walipata kiwiliwili cha
maiti ya msichana mdogo kikiwa bila miguu na mikono.Wawili hao walikiri
kwamba walipika mchuzi wa nyama ya viungo hivyo na kuvila.
Walishtakiwa kwa makosa ya kuharibu kaburi kwani nchini Pakistan hakuna sheria inayozungumzia hatia ya mtu kumla mwenzie.
Hata hivyo punde si punde polisi wamesema waliitwa na majirani wa jamaa huyo wakilalamikia uvundo mkali kutoka kwa nyumba yake.
Walipoingia chumbani humo Lo ! wakapata kichwa
cha mtoto.Kiwiliwili hakijulikani kililiwa au kapotelea wapi. Arif Ali
tena amekamatwa kwa mara ya pili na polisi wanaendelea kumsaka kakake.
Polisi wanaamini ndugu hawa walifukua maiti ya mtoto ambaye kichwa kilipatikana ndani ya makaazi yao.
Arif anamlaumu kakake Farman.Wawili hao waliwahi kuoa na hata wakajaliwa watoto, hata hivyo wake zao waliwatoroka kabla ya kukamatwa kwao na kufungwa jela kwa kisa cha awali.
>>>>Chanzo bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment