Mesut
Ozil atakuwa nje ya Uwanja kwa muda usiopungua Wiki 4 baada uchunguzi
wa kina kuthibitisha kuumia kwake kwa Musuli za Pajani (Hamstring).
Kiungo
huyo wa Arsenal mwenye Miaka 25 aliumia katika Dakika ya Pili tu ya
Mechi ya Jumanne Usiku ya UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Bayern Munich
ambayo walitoka Sare 1-1 na kutolewa nje ya Mashindano hayo lakini
alijikongoja kucheza hadi Haftaimu alipobadilishwa.
Ozil,
ambae alisainiwa kwa Dau la Rekodi kwa Arsenal ya Pauni Milioni 42.4
kutoka Real Madrid mwanzoni mwa Msimu huu, ataikosa tripu ya Arsenal
kwenda huko White Hart Lane Jumapili hii kucheza Dabi ya London ya
Kaskazini dhidi ya Mahasimu wao Tottenham kwenye Mechi ya Ligi Kuu
England.
Pia Ozil atazikosa Mechi na Chelsea, Swansea, Manchester City na Everton.
Hizo zote ni Mechi muhimu za Ligi Kuu England ambazo Arsenal ipo mbioni kupigania Ubingwa.
Mbali ya Mechi hizo, Ozil pia
ni hatihati kuikosa Mechi ya Nusu Fainali ya FA CUP dhidi ya Mabingwa
Watetezi wa Kombe hilo, Wigan Athletic, hapo Aprili 12 Uwanjani Wembley.
Tangu ajiunge na Arsenal, Ozil amefunga magoli 6 katika Mechi 35.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment