Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Rehema Saidi akielezea kitendo alichofanyiwa mtoto wake. Picha na Mary Sanyiwa

Newala. Kutokana na kumwamini mumewe, Rehema Saidi, mkazi wa kijiji cha Rahaleo, Kata ya Mkunya Wilaya ya Newala mkoani Mtwara, hakuwahi kutia shaka pale alipomwacha na watoto, wakati yeye alipolazimika kutoka kwenda sehemu yoyote kwa ajili ya shughuli za kifamilia.
Rehema na mumewe Juma Malolo waliishi na watoto wawili; mwenye umri wa mwaka ambaye walimzaa pamoja na mwenye umri wa miaka tisa ambaye (Rehema) alimzaa kwa mwanamume mwingine kabla ya kuolewa mara ya pili.
Mwanamama huyu anasema aliishi kwa raha mustarehe na familia yake na katika mazingira ya kawaida, hakuwahi kuwaza kutokea kwa kitendo alichokishuhudia Agosti, 14 mwaka jana, pale alipomkuta mumewe (Malolo) akimbaka binti yake (jina tunalihifadhi).
Rehema anasimulia kwamba siku ya tukio alikuwa akitoka sokoni alikokwenda kuchuuza mbogamboga kwa ajili ya kupata fedha za kujikimu yeye na familia yake.
“Niliporudi nyumbani nilifungua mlango bila hata ya kubisha hodi kwa sababu ni nyumbani kwangu na wala sikuwa na hofu ya jambo lolote…sikuamini pale nilipomkuta mume wangu akiwa anambaka mtoto wangu, kwanza nilipigwa na butwaa, nikapandwa na hasira, nilimvamia na kuanza kumpiga Niliumia sana kiasi siwezi hata kuhadithia aina ya maumivu niliyoyapata,” anasimulia kwa huzuni.
Anabainisha kuwa baada ya hapo, alitoka nyumbani hapo kuwaita majirani ili waweze kushuhudia kitendo hicho, lakini aliporejea hakumkuta mumewe kwani alikuwa ameondoka na kibaya zaidi alichukua fedha zilizotokana na biashara yake Sh40,000 ambazo zilikuwa ndiyo akiba pekee aliyokuwa amebaki nayo.
“Nilikwenda kwa baba wa mtoto kumwambia ili anisadie fedha ya kwenda mjini kutoa taarifa polisi lakini alisema hana fedha. Hivyo nilishindwa kwenda na hata hospitali kumpima, kwa sababu sikuwa na fedha tena ...nilibaki nyumbani huku nikilalamika kwa kitendo alichofanyiwa mwanangu,” anasema Mariam.
Anaeleza kuwa alikaa siku tatu bila kumwogesha binti yake kwa lengo la kutunza ushahidi wa kitendo alichofanyiwa na wakati huo alikuwa akitafuta fedha ili aende polisi na baadaye kumpeleka hospitali, lakini hakufanikiwa.
Mariam anasema baada ya siku tatu kupita huku akiwa amepoteza matumaini ya kupata nauli, alimwogesha mtoto huyo, hivyo ni dhahiri kwamba alipoteza ushahidi wa kitendo alichofanyiwa.
Ilikuwaje?
Rehema anasema siku ya tukio, Agosti 14 mwaka jana aliondoka nyumbani kwake saa 11 alfajiri kwenda shambani kwa Mzee Makwedu umbali wa kilomita tatu kutoka kijijini kwake, kununua majani ya kunde ili ayapeleke Mjini Newala kuyauza.
Anasema alimwacha mumewe na watoto wawili. “Nilimuaga mume wangu na kumwacha na watoto wote wawili, kwa kuwa nilimwacha na mtoto mchanga wa mwaka mmoja niliamua kufanya haraka ili asije akaanza kulia wakati sijarudi,” anasimulia na kuongeza:
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top