Mgogoro baina ya wakulima wa chai wa Bumbuli na Viongozi wa Chama cha wakulima wa chai cha Usambara (UTEGA) na mwekezaji wa kiwanda cha kusindika majani ya chai cha Mponde umeingia sura mpya baada ya wakulima hao kutishia kuandamana kupinga Mbunge wao, January Makamba kufikishwa mahakamani. Wakizungumza na Waandishi wa Habari, katika vijiji mablimbali vya Bumbuli, wakulima hao wamesema kuwa wanapinga hatua ya UTEGA kutaka kumfikisha mahakamani mbunge huyo wakishirikiana na muwekezaji. Wakulima hao walikitaka chama cha UTEGA na mwekezaji huyo kuacha mara moja kumhusisha Makamba na mgogoro huo ambao walisema ulianza mwaka 2003 wakati Mbunge huyo akiwa hayupo katika madaraka hayo. "Waliofunga kiwanda ni sisi wakulima na hatukufunga kwa kufuli bali tuliacha kwa hiari yetu kupeleka majani mabichi kiwandani kutokna na kudhulumiwa na viongozi wa UTEGA na mwekezaji huyo, Lushoto Tea Company ambayo inaendesha kiwanda cha chai cha Mponde," alisema Almasi Kassim, ambaye ni mwenyekiti wa Skimu ya Chai ya Mponde.
Kassim alisema kuwa wanakumbukumbu kuwa Mbunge huyo aliwasihi wakulima waache kuchukua hatua hiyo ambayo aliita hatua ngumu kwani itawaaathiri kiuchumi. Uchumi wa Bumbuli unategemea kwa kiasi kikibwa zao la chai ambalo linalimwa katika kata 13 kati ya kata 16 za Halmashauri hiyo. Imebainika kuwa hivi karibuni viongozi wa UTEGA na mwekezaji huyo walifanya kikao ambacho kiliazimia kuimpeleka mbunge huyo mahakamani kwa kusababisha kufungwa kiwanda cha Mponde. Katika hatua inayoashiria hasira za wananchi juu ya hali mbaya inayosababishwa na kufungwa kwa kiwanda hicho na serikali kuchelewa kutekeleza maamuzi ya Tume iliyoundwa na wadau kuchunguza mgogoro huo, wananchi hao wamesema kuwa wataingia kiwandani Machi 30, mwaka huu kukifungua kiwanda hico wenyewe kama serikali haitachukua hatua ifikapo tarehe hiyo.
Wakulima hao wamemwomba Rais aingilie kati mgogoro huo ili kuwaondolea wakulima hao adha ya kuonewa na mwekezaji na viongozi wa UTEGA. Mkulima mmoja wa kijiji cha Mpalalu, Ramadhani Hassan alisema kuwa wakulima walikifunga kiwanda wenyewe kwasababu wamechoka na dhuluma za mwekezaji kwa kushirikiana na viongozi wa UTEGA. "Kama ikifika taerehe hiyo serikali haijachukua hatua tutachukua hatua wenyewe na CCM isitegemee ina wanachama babada ya hapo," alisema Hassan. Mwingine, Noah Singano alisema wamengojea kwa hamu maamuzi ya serkali ya kuchukua kiwanda kama ilivyotangazwa na Waziri wa Kilimo, Christopher Chiza alipotembela wakulima.
Alisema kuwa serikali iache kumlea mwekezaji huyo ambaye amewadhulumu wakulima kwa miaka mingi. Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, Beatrice Msomisi amewataka wakulima hao kuwa wavumilivu wakati serikali ikichukua hatua kufungua kiwanda hicho.
Alisema kuwa hata serikali wameona wakulima hao ambao wamekaa na mwekezaji huyo kwa miaka mingi kuchukua hatua hiyo ya kuacha kupeleka majani ya chai mabichi kiwandani hapo sio wajinga. Msomisi alisisitiza kuwa hata Halmashauri pia imeathirika na kufungwa kwa kiwanda hicho na inafanya juhudi kiwanda kifunguliwe chini ya serikali.
>>>>> hisan ya raisa said, bumbuli
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment