Ramires
na Willian wako huru kuitumikia Chelsea leo kwenye mechi ya marudiano
ya Champions League hatua ya 16 dhidi ya Galatasaray, mchezo ambao
utapigwa jumanne hii kwenye dimba la Stanford Bridge.Wachezaji hao walitolewa nje ya uwanja wakati timu hiyo ilipokubali kupigo cha 1-0 kutoka kwa Aston Villa siku ya jumamosi.
Ashley
Cole anasumbuliwa na goti na hakuwepo kwenye kikosi kilichoshiriki
mazoezi ya pamoja jana jumatatu lakini David Luiz alikuwepo na huenda
akaanza kwenye kikosi cha kwanza pale Stamford Bridge kwenye mchezo wa
marudiano ambapo awali timu hizo zilitoka sare ya 1-1.David Luiz coanaweza kucheza nafasi ya Nemanja Matic ya kiungo wa kati.Naye mshambuliaji wa zamani wa Blues Didier Drogba, 36, anatarajia kuanza katika kikosi cha Galatasaray huku Mohammed Salah akiikosa mechi hiyo kwa sababu aliwahi kuichezea Basel mwanzoni mwa mashindano hayo kabla ya kutua Chelsea.
Naye
boss wa Real Madrid Carlo Ancelotti hatompumzisha kiungo wake Cristiano
Ronaldo katika mchezo wa Champions League dhidi ya Schalke, kwa ajili
ya El Clasico.
Meneja
huyo amethibitisha kuwa Ronaldo, 29, ataanza kwenye kikosi cha kwanza
katika mchezo wao wa marudiano hatua ya 16 dhidi ya FC Schalke.
Mchezo
huo utapigwa leo kwenye dimba la Santiago Bernabeu. Katika mchezo wa
awali uliopigwa Ujerumani Real iliibuka na ushindi wa 6-1.
Spanish leaders Real host arch-rivals Barcelona, who are third, on Sunday.
Mechi zote zitanza majira ya saa tano kasoro majiara ya Afrika mashariki (22:445)
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment