Sintah & Juma Nature.
Kati ya break-up zilizowahi kumake headlines namba moja ni hii
hapa,sababu hadi ilikuwa ukimuuliza mtoto mdogo anaweza kukuambia,Sintah
akiwa ni muigizaji maarufu sana hapa Town,wakati Juma nature ndio mkali
wa Bongo Fleva waliweza ku-date kwa kipindi kirefu kidogo na hii ndio
ilikuwa celebrity couple maarufu,ilikuja kufikia Tamati ya penzi lao
kutokana na kile kinachosemekana kuwa ni kutoaminiana kwa wawili
hawa,hadi kufikia wakati Juma Nature kumuimbia mpenzi wake wimbo
uliokuwa unahusu kuvunjika kwa mahusiano yao.
Wema Sepetu & Chaz Baba.
Wakati ambapo jina la Wema Sepetu halikuwa kubwa kama ilivyo hivi
sasa,kipindi hicho kabla hata ya story za Diamond hazijawa talk of the
town wapenzi hawa wawili walikuwa ndio wako katika mapenzi motomoto,Chaz
Baba akiwa ni msanii Mwimbaji maarufu wa bendi,huku Wema Sepetu ndio
alikuwa Miss Tanzania mwaka 2006.
Haikujulikana ni nini haswa chanzo cha break-up yao,ila baada tu ya Chaz
Baba kuachwa huku bado akiwa anampenda Wema,Wema Sepetu ndipo alikuwa
amesha anguka katika Penzi Jipya kabisa la Naseeb Abdul maarufu kama
Diamond Platnumz.
Diamond Platnumz & Wema Sepetu.
Kwa mujibu wa Wema Sepetu mwenyewe,inasemekana kuwa breakup hii
ilisababishwa na Jokate,sababu muda walipokuwa wapenzi na mambo yao
yalikuwa yanaenda vizuri tu,na hawakuwa na ugomvi wowote uliokuwa
unaendelea kati yao,ila mbali na rumors alizokuwa anasikia za hapa na
pale na kutoziamini,siku ikafika ndipo alipowakuta wawili hao wakiwa
pamoja.
Wema na Diamond mbali na kuwa wameweza kuachana mara nyingi katika
kipindi chao cha mahusiano,inaonekana wawili hao wanamapenzi ya
kweli,sababu baada ya muda kupita huku kila moja akiwa anakula
vyakwake,mwisho wa siku walichoka ku-pretend na kuweza kurudiana hadi
hivi sasa penzi lao likiwa bado lipo moto moto.
Jokate & Diamond Platnumz.
Hii ni moja ya couple iliyowahi kudumu kwa muda mfupi kweli hapa
town,ila rumors has it kuwa wawili hawa walikuwa wana-date kisiri
sana,haikujulikana kwa hukika walikuwa wapenzi kwa muda gani ila kipindi
Diamond Platnumz wana misunderstanding na Wema ndipo Jokate alipoingia
kati na kuweza kuchukua nafasi lakini wakati huo huo bado Diamond
alikuwa bado yupo Officialy na Wema.Baada ya Wema Sepetu kuwakuta live
Diamond na Jokate ndipo inasemekana huo ulikuwa mwisho wa mahusiano yao.
Hasheem Thabit &Jokate.
Hasheem Thabit akiwa ni mchezaji wa kikapu wa kulipwa huko marekani
kutoka hapa Tzee, nae ali-fall katika penzi na Jokate Mwegelo,ingawa
mahusiano yao yalikuwa si ya public sana,labda kutokana na Hasheem
Thabit kuhamisha makazi yake huko nchini marekani wakati Jokate alikuwa
hapa Tanzania,ilikuwa vigumu sana kuwakuta wawili hawa mara kwa mara.
Baada ya muda kupita habari za hapa town zilikuwa ni kwamba Jokate na
Hasheem Thabit wali break-up,alipoulizwa moja kwa moja Jokate aliweza
ku-confirm habari hizo na sababu za break-up hiyo zilikuwa zinasemekana
kuwa ni umbali kati ya wawili hao,huku kila mmoja kutomwamini
mwenzake,ila rumors has it kuwa ni kwa sababu Jokate alikuwa anatoka na
Diamond.
Diamond Platnumz & DVJ Penny.
Baada ya Diamond kuachana na Wema,Diamond aliangua kwenye penzi la Dvj
maaruf hapa Town,Dvj Penny,mapenzi yao yaliweza kudumu kwa miezi
kadhaa,wawili hawa walionekana wamefall kabisa moja kwa moja,waliiva
sana katika kipindi chao cha mahusiano hadi pale Diamond alipoamua
kurudi kiroho safi tu, kwa mpenzi wake wa Zamani Wema
Sepetu.Haikujulikana ni nini haswa chanzo cha break-up yao,ila rumors
has it kuwa diamond alikuwa bado anampenda Wema Sepetu na hakuweza
kuficha hisia zake kwa Wema kipindi yupo na Dvj Penny.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment