MWANAMUZIKI
mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ anayetumikia kifungo cha
maisha jela na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kwa kuwanajisi watoto
tisa, wana furaha upya baada ya mwanga wa kuweza kurudi uraiani
kuchomoza tena, wakili wao, Mabere Nyaucho Marando amezungumza na Uwazi.
KASORO HUKUMU YA MWANZO
Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Marando alisema kwamba katika
kesi ya Babu Seya na mwanaye iliyosikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Dar aligundua kuna vielelezo muhimu ambavyo
havikuambatanishwa hivyo kuwa vigumu kwake kuviingiza na kuvitetea
katika ngazi ya mahakama ya rufaa iliyoshindilia adhabu dhidi ya wawili
hao.
Marando alisema mwanga mwingine wa
kupitiwa upya wa mashitaka yao umekuja baada ya kuwepo kwa kesi mpya
inayofanana na ya akina Babu Seya kwa asilimia mia moja. Alisema kesi
hiyo ipo kwenye hatua ya mwisho ambapo ushindi wake utamfanya apate
nguvu ya kurudi mahakamani kuwatetea wafungwa hao waliohukumiwa mwaka
2004.
DIRA KWENYE KESI HIYO “Kuna kesi
mahakama kuu kanda moja nchini inayotetewa na wakili maarufu (jina
tunalo). Hii kesi inafanana sana na ya akina Babu Seya. Uzuri wake ina
dalili zote za washtakiwa kuibuka na ushindi wa kishindo. MAHOJIANO
Mazungumzo kati ya Marando na Uwazi yalikuwa hivi:
Uwazi: Lakini mheshimiwa kesi ya Babu
Seya si ilifika katika rufaa mara tatu na wakashindwa na ulisema hakuna
namna tena, sasa itakuwaje kurejeshwa tena huko? Marando: Ni kweli,
lakini ni jambo linalowezekana.
Nimesema kama hiyo kesi ninayoitaja
watashinda na wanaweza kushinda, basi mimi nitaenda kwa Nguza na
kumwambia wazo langu, akikubali nitaiandikia barua mahakama ya rufaa
kuomba kupitiwa tena kwa yale mashitaka, nitajenga hoja.
Uwazi: Hiyo kesi unayoingoja hukumu yake
inahusu nini? Marando: Inahusu kubaka na kulawiti, ni kama hii ya Babu
Seya na wanawe. Hakuna tofauti. Sasa washitakiwa wale wakishinda ndipo
hoja inapokuja, kwa nini vipengele vilevile viwatie hatiani akina Babu
Seya wengine viwaweke huru, ndivyo inavyokuwa katika kesi. Uwazi:
Ukiwaandikia mahakama ya rufaa wakakubali, majaji walewale watasikiliza
ombi lako?
Marando: Hilo ni la mahakama lakini
idadi inaweza kuongezwa na kufikia majaji sita au saba.Uwazi: Una
hakika utashinda na kukubaliwa? Marando: Kama nilivyokueleza, ikipita
ile kesi halafu mahakama ya rufaa wakakubali kupitia tena jalada, nina
uhakika wa kushinda.
ANALIPWA NA NANI? Wakili huyo maarufu
alisema yeye aliwatetea wanamuziki hao bure kwenye kesi yao ikiwa
katika ngazi ya mahakama ya rufaa baada ya kusoma jalada lenye kurasa
1,362 ambapo aligundua kuwa kuna nyaraka kadhaa ambazo
hazikuambatanishwa katika Mahakama ya Kisutu ambazo zingeweza kuwaokoa
na kifungo wateja wake.
“Unajua kesi inapokuwa mahakama ya
rufaa, majaji wanachofanya ni kupitia jalada si kusikiliza, hivyo
haiwezekani kuambatanisha vielelezo vipya,” alisema Marando ambaye
anajipambanua kuwa awali alishinda nusu kwa kuwatoa nje watoto wa Babu
Seya, Mbangu na Francis Nguza ambao nao walihukumiwa kifungo cha maisha
jela kwa kosa moja na wafungwa hao.
HUKO NYUMA Juni 25, 2004 Hakimu
Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, Addy Lyamuya aliwatia
hatiani kwa ubakaji na ulawiti Babu Seya na wanawe Papii Kocha, Mbangu
na Francis. Januari 27, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga
hukumu hiyo.
Wakili Marando akapeleka suala hilo
Mahakama ya Rufaa Tanzania ambako Mbangu na Francis waliachiwa huru na
yeye kutangaza kwamba ameshinda nusu. Babu Seya na wanawe walidaiwa
kutenda makosa 10 ya kubaka na kulawiti watoto hao kati ya Aprili na
Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza ya Kwaremmy, Dar es Salaam.
>>>>Uwazi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment