MTU mmoja mkazi wa eneo la Sakina jijini
Arusha aliyefahamika kwa jina la JAPHET MINJA amemwagiwa kitu
kinachodhaniwa kuwa ni tindikali usoni na mkononi na watu wasiojulikana
katika eneo la Shamsi kata ya Elerai na kumsababishia majereha.
Akizungumza katika hospitali ya Selian
alikolazwa kwa matibabu MINJA ambaye ni fundi ujenzi amesema ametokewa
na tukio hilo jana majira ya saa tatu asubuhi katika eneo la shamsi
Drive in wakati akitoka nyumbaji kwake akiwa ndani ya gari ambapo
alisimamishwa na watu waliomtaka kuongozana nao kwa ajili ya kufanya
biashara na ghafla wakiwa njiani walimgeuka.
Daktari wa zamu aliyempokea mgonjwa huyo GODBLESS MASAWE amesema walimpokea jana asubuhi akiwa na fahamu lakini baadae hali ilibadilika na kulazimika kumpeleka katika chumba cha wagonjwa mahututi na kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.
Jeshi la polisi mkoani Arusha kupitia kwa kamanda msaidizi ASP JAPTET LUSINGI amesema bado hawana taarifa kuhusiana na tukio hilo.

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment