Agnes Gerald ‘Masogange’.
Mtandao
wa wauza madawa ya kulevya unazidi kupukutika Bongo kufuatia madai ya
kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kujishughulisha na ubebaji ‘punda’ wa
biashara hiyo haramu, Hivi
karibuni, Video Queen wa Wimbo wa Masogange, Agnes Gerald ‘Masogange’
amedaiwa kunaswa nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ akiwa na kilo mia moja na
hamsini za unga unaoaminika ni sehemu ya madawa ya kulevya. Ameshapanda
kortini mara moja Ijumaa iliyopita.Wakati
Masogange akisota Sauzi kwa madai hayo mazito, habari ya mjini kwa sasa
ni ya mtalaka wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Mohammed ’Z-Anto’,
Sandra Khan au Binti Kiziwi kudaiwa kutupwa jela miaka mitano kwa sakata
la ‘unga’.
Sandra Khan 'Binti Kiziwi'.
HABARI YA MJINI KWA SASA NI BINTI KIZIWI
Kuanzia Alhamisi iliyopita,
habari zilizoligubika Jiji la Dar ni kuwa Binti Kiziwi amenyongwa
nchini China baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya
kulevya.
Kwa mujibu wa mitandao, Binti Kiziwi alinyongwa wiki mbili zilizopita.
Hata hivyo, mitandao hiyo
haikusema kama mrembo huyo alinyongwa hadi kufa au la! Sheria za hukumu
hiyo, mwenye hatia anatakiwa kunyongwa hadi kufa.
Sharifa Mahamoud (27)
Melisa Edward
Saada Ally Kilongo (26),
UKWELI WA BINTI KIZIWI NI HUU
Baada ya kusambaa kwa manenomaneno hayo, Ijumaa Wikienda liliingia mtaani kuisaka familia ya Binti Kiziwi lakini bila mafanikio.
Kwenye makazi ya mama yake,
Buguruni, Dar, majirani walisema mzazi huyo amehama baada ya kufunga
ndoa siku chache kabla ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
IJUMAA WIKIENDA LAZIDI KUCHIMBA
Ijumaa Wikienda lilizidi
kuzama ndani katika kuchimbua tetesi hizo ambapo lilifanikiwa kumpata
ndugu wa kiume wa Binti Kiziwi na kufanya naye mazungumzo kama
ifuatavyo:
Wikienda: Samahani, nimeambiwa wewe ni ndugu wa Binti Kiziwi, ni kweli?
Ndugu: (huku akitaja uhusiano wao) Ni kweli, nikusaidie nini?
Wikienda: Kuna manenomaneno
kwamba Binti Kiziwi amenyongwa nchini China baada ya kupatikana na
hatia ya kukutwa na madawa ya kulevya, ni kweli?
Ndugu: Sijui hizo habari watu wanazipatia wapi?! Watanzania wana maneno sana. Si kweli ndugu mwandishi.
Wikienda: Ukweli ni upi?
Ndugu: Kwanza kabisa Binti
Kiziwi hakukamatiwa China, alikamatiwa Hong Kong, kwa sheria za kule mtu
akipatikana na hatia ya kukutwa na ‘unga’ anahukumiwa jela tu.
“Binti Kiziwi amehukumiwa miaka mitano jela Hong Kong, na si China. Watu wajue hilo na miaka mitano si mingi, atatoka.”
Wikienda: Nashukuru sana kwa ushirikiano ndugu yangu.
Ndugu: Asante, waambie Watanzania waache kuongeaongea sana
EMU WA KANUMBA NAYE ASOTA RUMANDE
Msichana
anayejulikana kwa jina la Saada Ally Kilongo (26), maarufu kama ‘Demu
wa Kanumba’ yeye bado anasota kwenye Gereza la Segerea, Dar kwa tuhuma
za kukutwa na madawa ya kulevya yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi
ya shilingi milioni 170.
Saada alidakwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Juni 24, mwaka huu.
Kesi yake ilisikilizwa kwa mara ya kwanza, Juni 29, mwaka huu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam.
Mdada
huyo mkazi wa Mbezi Beach, Dar aliwahi kutoka kwenye Gazeti la Ijumaa
la Desemba 9, 2011 ukurasa wa mbele kwa kichwa cha habari kisemacho: SAA
7 USIKU KANUMBA AGANDANA NA DEMU.
Demu huyo ambaye
wakati huo alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama,
Dar (alimaliza mwaka jana), picha yake akiwa na marehemu Kanumba
ilipigwa Desemba 2, 2011 ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar ambapo
kulirindima Tamasha la Usiku wa Kiafrika lililopambwa na mkali wa dansi
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ipupa Nsimba ‘Fally Ipupa’.
MSANII BONGO MUVI ‘ASUBIRI KITANZI’ MISRI
Wakati mlolongo wote ukiwa
hivyo, mrembo aliyewahi kushiriki filamu Bongo, Sharifa Mahamoud (27)
naye anashikiliwa katika gereza moja nchini Misri wakati kesi yake ya
kukamatwa na madawa ya kulevya ikirindima nchini humo.
BALOZI WA TANZANIA -MISRI AZUNGUMZA
Kwa mujibu wa Balozi wa
Tanzania nchini Misri, Mohammed Haji, Mei 18, mwaka huu, Sharifa na
nduguye, Abdallah Salum (28), wote wakazi wa Magomeni, Dar, walinaswa na
unga jijini Cairo wakitokea Dar.
Mei 26, walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza. Madawa waliokutwa nayo ni heroine kilo saba (gharama ya fedha haikutajwa).
Kwa sheria za Misri, kosa
la kukutwa na madawa ya kulevya ni kunyongwa hadi kufa. Lakini kwa
mujibu wa Balozi Salum, hana kumbukumbu za raia wa kigeni aliyewahi
kuhukumiwa kunyongwa nchini humo kwa kosa hilo.
Balozi alisema: “Endapo
watapatikana na hatia kwamba kweli dawa hizo zilikuwa zao, hili litakuwa
doa la kwanza kwa nchi yetu (Tanzania) hapa Misri.
Kwa mujibu wa Sharifa
wakati akihojiwa na TV ya Misri, alishangaa kuona begi lake likiwa na
madawa ya kulevya baada ya kukamatwa na kwamba aliingia nchini humo
kumtafuta binamu yake.
chanzo:globalpublishers
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment