Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
PICHA YA STUDIO ZA CLOUDS FM BAADA WATANGAZAJI KUZICHAPA
Kama ulikuwa Hewani siku ya jana katika kipindi maarufu kabisa (XXL), ndani ya Stetion maarufu hapa Tz yaani nazungumzia CLOUDS Fm utaelewa nini ninachozungumzia mpaka sasa.
Katika hali isiyotegemewa jana watangazaji watatu maarufu kama, DJ FETTY, ADAM MCHOVU na B12 waliziweka ndani ya studio za Clouds live huku wakisahau kuwa Wasikilizaji wanawasikia mwanzo mwisho wanachokifanya huko ndani ya studio. Sakata hilo limesababisha na kutoelewana baina ya hawa watangazaji juu ya mauzo ya Albam ya Fiesta! 
Sasa leo watu mbalimbali na wasikilizaji walikuwa nataka kujua nini zaidi kilitokea kupitia kipindi cha Hekaheka, chanzo cha ugomvi hasa ni nn?
Baada ya message nyingi sana kwenye kipindi cha hekaheka ilibidi wahusika wanyanyue simu zao kuwatafuta Adam, Fetty na B12 kujua nini kilichosababisha kuchapana makonde wakati bado kipindi kikiwa hewani.
 Muhusika alinyanyua moja kwamoja simu na kumpigia B12 ambaye alikataa kabisa kueleza chanzo cha sakata hilo la kutwangana huku akisema mambo yote yapo kwa uongozi...
Simu ya pili ilimuendea ADAM MCHOMVU ambaye pia aligoma kuelezea kilichotokea jana, baada ya Muda mfupi Adam alimkabidhi Dem wake ili azungumze na mwandishi, huku akijua kwamba harikodiwi kumbe yupo hewani, alikiambia kipindi cha hekaheka kwamba ADAM amemaind na hataki kuongea na simu!! 
Simu ya tatu ilienda kwa DJ FETTY, Ambapo iliita bila majibu kwamba ilikuwa haipatikani..
Chanzo kinasema kwamba baada ya ugomvi, vifaa mbalimbali vya studio vimeharibiwa wakati wa ugomvi huo kama MIC, COMPUTER Meza nk.  Endelea Kufuatilia Hapa ili ujua ni hatua Gani watachukuliwa watangazaji hawa kwa kukosa utovu wa Nidhamu....
Chanzo-tanzanianewz.com
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top