Home
»
Kitaifa
» Waziri Simbachawene Aagiza Machinga waondolewe Kariakoo....Asema Rais hakumaanisha warudi
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga katika maeneo ya soko la Kariakoo na barabarani, hususan karibu na barabara za mabasi ya mwendo kasi.
Akizungumza jana na Kamati ya Bunge, Waziri huyo wa TAMISEMI alisema kuwa kurejea kwa wafanyabiashara hao katika maeneo hayo kumeleta usumbufu mkubwa na uchafu wa mazingira katika maeneo ya jiji.
“Namuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awaondoe na asilegeze kamba,” alisema Waziri Simbachawene.
Alisema kuwa hali hiyo imetokana na tafsiri isiyo sahihi ya agizo la Rais John Magufuli alipokuwa ziarani Mkoani Mwanza.
“Wala agizo la Mheshimiwa Rais halikumaanisha hicho. Mheshimiwa Rais alisema tuwatafutie maeneo mbadala ambao wapo maeneo kama ya Mwanza na walikuwa wanafanya biashara ya kuuza nguo, akizungumzia wale particular group walioko pale Mwanza. Kwa Dar es Salaam tulishamaliza huko,” alisema.
Aidha, alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha hakuna hata machinga mmoja atakayeonekana akifanya biashara katika maeneo ya barabara za mabasi yaendayo kasi.
Aigizo hilo la Waziri Simbachawene liliungwa Mkono na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge ambao walisema kuwa hali ya soko la Kariakoo imekuwa mbaya kutokana na kuzagaa kwa machinga.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 9 201609 Sep 20160
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo September 09 201...Read more ?
- Viongozi wa Afrika Mashariki Waigomea Ulaya....Wajipa Miezi Mitatu Kuutafakari Mkataba wa EPA09 Sep 20160
JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC), imeiomba Jumuiya ya Ulaya (EU), iipe muda wa miezi mitatu kuju...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Majibu ya Waziri mkuu Majaliwa Leo Bungeni kuhusu wahusika wa mauaji ya askari08 Sep 20160
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaendelea kukutana na wadau tofauti wanaohusika na ...Read more ?
- Makamu wa Rais: Viongozi Na Watumishi Wa Umma Kuchukuliwa Hatua Kali Iwapo Watabainika Kukiuka Taratibu Za Kazi08 Sep 20160
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Sekretarieti ya M...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment