March 14, 2025 02:16:42 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kusema kuwa baada ya kuachana na mpenzi wake wa zamani Nay wa Mitego ambaye alimuweka wazi kwa jamii na kuja kuachana baada ya muda mfupi alikuwa mwoga tena kumuweka wazi mpenzi wake mpya.

Shamsa Ford alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ na kusema kuwa alikuwa mwoga kumuweka wazi kwa jamii mpenzi wake mpya lakini kwa kuwa mapenzi yamemzidi imebidi sasa amuweke wazi, kwani anasema mapenzi huwezi kuyaficha.

“Mwanzo kweli nilikuwa naogopa lakini mapenzi yakizidi huna namna inabidi tu ujiachie, ni kweli mpaka sasa tayari ameshanitolea mahari nyumbani” alisema Shamsa Ford

Katika kusherehekea siku ya kuzaliwa Shamsa Ford alitumia nafasi hiyo kumtambulisha mpenzi wake mpya ambaye anafahamika kwa jina la Chid Mapenzi ambaye mara kadhaa alikuwa akisema ni mtu anayeshirikiana naye kwenye biashara tu.

eatv.tv


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
03 Aug 2016

Post a Comment

 
Top