WAKATI Chama cha wananchi CUF ambacho ni chama kikuu cha Upinzani visiwani Zanzibar kikiwa kimesusia uchaguzi wa marudio ambao unafanyika Marchi 20 ya mwaka huu,Baraza la Waislam (BAKWATA) limesema marudio ya uchaguzi huo ndo njia ya kipee ya kurudisha amani visiwani humo..
Katika hatua nyingine, Baraza hilo limeipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jitihada mbalimbali inazofanya za kuimarisha nidhamu, kubana matumizi na kukuza uchumi.
"Pia tunaipongeza serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mh. John Magufuli, kutokana na hatua mbali mbali inazozichukua zenye lengo la kuimarisha nidhamu hasa kwa watumishi wa umma, hatua mabazo zimeanza kuleta tija kubwa ka taifa letu kama wote hivi leo tunavyoweza kushuhudia jinsi pato la serikali likongezeka mwezi hadi mweziβ, alisema Sheikh alhadj Mussa Salum na kuongeza;
βAidha tunaipongeza kwa dhamira yake ya kubana na kupunguza matumizi ya serikali, na badala yake kuelekeza fedha kwenye huduma za jamii na watanzania tumeshaanza kunufaika na huduma hizo kama vile suala la elimu bure."
Post a Comment
Post a Comment