Home
»
general news
» Waziri Nape Ataja Sababu Za Kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama “MAWIO”.
Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa leo 17 Januari, 2016 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati alipokutana na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Nnauye amesema kuwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa tarehe 15 Januari, 2016 Serikali imelifuta Gazeti hilo ikiwa ni uamuzi uliotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).
Alieleza kuwa, hatua ya kulifuta gazeti hilo inazuia pia gazeti la Mawio kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.
‘’Serikali kwa masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi yetu’’, alisema Nnauye.
Aidha, alifafanua kuwa hatua hiyo ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari, 2016 kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na makala katika gazeti lake, bila mafanikio.
"Msajili wa magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na Mhariri wa gazeti hilo mara nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti,
"Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote.
"Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo’’ alisisitiza Mhe. Nnauye.
Katika hatua nyingine, Waziri nape alitoa pongezi kwa Vyombo vyote vya habari nchini vinavyozingatia maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za nchi.
‘’Kwa namna ya pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari ambavyo vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na kutoa ushirikiano kwa Serikali na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja na wahariri wa magazeti ya; Mwananchi Tanzania, Mtanzania, The East African, Magazeti ya Daily News na Habari Leo, Uhuru na mengineyo’’, alisema Mhe. Nnauye.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Jamaa Aliyejitosa Zoo Aliwe na Simba Laivu Alikuwa Anadai Mwisho wa Dunia Umefika...23 May 20160
Inasikitisha kwakweli, ameokolewa.... na simba walioanza kumla waliuwawa. aliingia kwenye jumba ...Read more ?
- Watumishi HEWA Waziponza Benki.......Benki za Dar es Salaam Zalimwa Barua Kurejesha Mamilioni ya Shilingi23 May 20160
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 21 kwa benki zilizokuwa zikitumika kuwek...Read more ?
- Waziri Nchemba Afanya Ziara Ya Kushtukiza Saa Saba Usiku Machinjio Ya Ukonga Mazizi Na Kufukuza Viongozi Wote Wa Machinjio12 Feb 20160
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mwigulu Nchemba amefanya ziara ya Kushtukiza saa saba usiku...Read more ?
- Askofu Gwajima, Sheikh Wa Mkoa Dar Wakwama Kumjulia Hali Mufti12 Feb 20160
Jopo la Madaktari wanaomtibu Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir wamezuia ...Read more ?
- Siku 100 za Rais Magufuli: Hospitali Ya Muhimbili Yang'aa, Mapato Yapaa na Upatikanaji wa Dawa Waongezeka Kwa Asilimi 9611 Feb 20160
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam imesema ndani ya siku 100 z...Read more ?
- Lowassa Atakiwa Kuvisaidia Vyombo Vya Dola Kukabiliana na Tishio La Kundi la al Qaeda Kuingia Nchini10 Feb 20160
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed amemtaka Wa...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment