Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Ndugu zangu wana JF kama kuna wabunge majipu basi mbunge wangu wa Ubungo Mh Kubenea ni jipu na linaitaji kupasuliwa.
Naamini wana Ubungo mtakubaliana na mimi kuwa kwa miaka hii mitano tumekula shoti kama sio loss.
Ubungo maji kwa wiki yanayoka mara moja wakati mwingine yanaweza yasitoke kabisa, Ubungo imejaa vibaka yani ukisahau jeans yako nje ndo nitolee, Ubungo wafanyabiashara ndogo ndogo wanapata shida, Ubungo barabara za ndani hazipitiki, Ubungo kuna kila aina ya matatizo.
Cha kushangaza tangu tumchague Kubenea sijasikia akiongelea matatizo ya Ubungo zaidi ya kupambana na Zitto , Makonda na wengine katika magazeti yake.
Mbunge huyu ata akichangia bungeni ni pumba tupu Ubungo tumezoea wabunge wenye uwezo wa kujenga hoja sio huyu Kubenea pamoja na kwamba Mnyika hakufanya makubwa sana ila afadhari yeye alikuwa ni mbunge wa kitaifa zaidi hakuna ubishi wanaubungo kwa Kubenea tumekula loss.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
30 Jan 2016

Post a Comment

 
Top