Home
»
Matukio
» Mwanamke Akutwa Kwenye Paa La Jengo La Wizara Ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanamke mmoja amepanda katika paa la jengo la Wizara ya Fedha na Mipango huku tukio hilo likizua sintofahamu kwa wafanyakazi wa wizara hiyo na wapita njia.
Tukio hilo lilitokea jana Dar es Salaam majira ya asubuhi ambapo mwanamke huyo anayedaiwa kuwa raia wa Kenya alipanda juu ya paa hilo na kuanza kupiga kelele.
Katika tukio hilo, inadaiwa mwanamke huyo aliwasili katika eneo hilo la wizara akionekana kama mmoja wa wananchi ambao walikwenda kwa ajili ya kupatiwa huduma, lakini baada ya muda alionekana akiwa juu ya paa huku akipiga kelele.
Mwanamke huyo aliyekuwa amebeba mkoba, ambaye haikufahamika mara moja nia yake ya kupanda juu ya paa hilo, ilimchukua saa kadhaa akiwa juu na pale walinzi wanaolinda ofisi za wizara hiyo walipokwenda katika eneo hilo na kumwomba ateremke aligoma.
Hata hivyo hali hiyo ilionekana kutowakatisha tamaa walinzi hao wanaolinda majengo ya Wizara ya Fedha na Mipango yaliyopo mita chache kutoka Ikulu ya Dar e Salaam, ambao walikwenda tena wakiwa na ngazi na kuanza kumbembeleza ambapo jaribio hilo lilifanikiwa na mwanamke huyo kuteremka.
Wakati mwanamke huyo akiwa juu ya paa, wananchi waliokuwa chini walianza kumuuliza maswali, lakini hakusikika majibu yake kutokana na kelele za watu ambao kila mmoja aliimuuliza swali lake.
Hata hivyo mmoja wa askari wa kikosi cha Usalama Barabarani ambaye alisogea kwa karibu kumuuliza mwanamke huyo, alisema kuwa alimwambia amechukua uamuzi huo kutokana na kuteswa na askari nchini Kenya.
“Tukio hili ni la ajabu na linaibua maswali… hivi inakuwaje kwa jengo kama hili la wizara ambalo lipo jirani na Ikulu mtu anapanda juu na walinzi wapo?
“Hii inasikitisha sana na ni ajabu kwa kweli, ipo siku tutakuta watu wanaingia Ikulu na kufanya mambo ya ajabu kwa viongozi wetu,”alisema mmoja wa wananchi waliokuwa katika eneo hilo ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini.
Alipotafutwa Msemaji wa wizara hiyo, Ingiahedi Mduma ili kuzungumzia suala hilo, alisema kwa sasa yupo mjini Dodoma katika maandalizi ya vikao vya Bunge na hana taarifa ya tukio hilo.
Mwanamke huyo akizungumza na watu waliokusanyika lakini alikuwa hasikiki vizuri maneno aliyokua akiongea kutokana na wananchi waliokusanyika kumuuliza maswali mengi kwa wakati mmoja.
Polisi akiwa pembeni ya uzio wa majengo ya wizara ya fedha na mipango mara baada ya mwanamke huyo kuwa juu ya paa la nyumba hizo. Baada ya muda wafanyakazi wa wizara hiyo walimwekea ngazi na kumshusha ili kumhoji zaidi nini kimemfanya apande juu ya paa la majengo hayo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment