Home
»
SIASA
» Lowassa kumnadi Godbless Lema Arusha Mjini Jumamosi hii....Pia Atalitumia Jukwaa Hilo Kuwashukuru Watanzania
Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa anatarajiwa kupanda jukwaani Jumamosi kumuombea kura mgombea wa ubunge wa Chadema Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema.
Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za ubunge katika jimbo hilo uliofanyika Soko Kuu jana, Lema alisema Lowassa atazungumza na Watanzania na kuwashukuru pia kwa kura nyingi walizompa.
Awali, mbunge mteule wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alieleza kuwa Lowassa na viongozi wa Chadema watatoa tamko zito siku hiyo na kuwataka wakazi wa Arusha na Watanzania kutega masikio.
Lema ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwataka wakazi wa Arusha, kutokatishwa tamaa na kuendelea kuwa na huzuni kutokana na matokeo ya urais yaliyotangazwa na kuwa bado kuna harakati za chama hicho kusaka haki.
“Ndugu zangu msikate tamaa, tumesikia wengine wametupa shahada zao, hapana, kazi ndiyo imeanza na lolote linaweza kutokea kwa uwezo wa Mungu,” alisema.
Alisema huzuni ya matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), haipo kwa wananchi tu, bali hata wajumbe wote wa kamati kuu.
“...Kwenye kikao cha kamati kuu, kuna wajumbe walimuomba Lowassa atoe tamko... kama angetoa tamko la kupinga matokeo na kukubali watu kuingia mitaani, Tanzania ingekuwa imeingia katika machafuko makubwa.
“Tunaendelea kutumia taasisi za kimataifa kudai haki, ndiyo sababu mnaona Zanzibar wameshindwa kujitangazia matokeo, hii ni kazi kubwa ya Ukawa,” alisema.
Katika mkutano huo, Lema alieleza njama alizosema zinapangwa kumnyima ushindi na akaonya kuwa hatakuwa tayari kuona ameshinda lakini mwingine akatangazwa kushinda.
“Najua Arusha nitashinda kwa kura nyingi, lakini kama wakitaka kunipora ushindi sitakubali,” alisema Lema.
Aliwaomba wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi Desemba 13 kumpigia kura nyingi, ili pia kuwezesha Chadema kupata viti viwili zaidi vya wabunge wa viti maalumu.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Profesa Lipumba Asema Hana mpango wa kuhama CUF wala kuanzisha chama Kingine ........Ataja Sababu Zilizomfanya Amkatae Lowassa08 Sep 20160
Aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema hana mpango wa kuhamia chama choch...Read more ?
- Msajili amlima Barua Maalim Seif kuhusu sakata la Lipumba01 Sep 20160
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini imemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananch...Read more ?
- Breaking News: Mbowe Atangaza Kuahirisha Maandamano ya Oparesheni UKUTA Yaliyokuwa Yamepangwa Kufanyika Kesho31 Aug 20160
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Opare...Read more ?
- Hotuba ya Edward Lowassa alipokuwa Iringa Jana25 Aug 20160
Leo(Jana) nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza kuwa tu...Read more ?
- Prof Lipumba:Sihusiki na Vurugu zilizotokea Katika Mkutano wa CUF23 Aug 20160
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesema hausiki na fujo wala vurugu zilizotokea ...Read more ?
- Mbunge kizimbani kwa maneno ya uchochezi23 Aug 20160
MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mussa Mbarouk amefikishwa katika Maha...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment