March 17, 2025 02:45:48 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

1

Eva Carneiro (42) akiwa na mumewe Jason De Carteret wakati wa harusi yao.
EVA (2)
...Wapenzi hao wakiwa na furaha baada ya kufunga ndoa.
EVA (3)
...Wakionyeshana upendo kwa kubusiana.
EVA (4)
Kipa wa zamani wa Chelsea, Mark Schwarzer ambaye kwa sasa anachezea Leicester City alihudhuria sherehe hiyo.
EVA (5)
Eva akiongozana na baba yake kuelekea kanisani.
EVA (6)EVA (7)
Padri akiongea na Eva pamoja na baba yake kabla ya ibada.
EVA (8)
Daktari Eva akiwa na Mourinho wakati akiitumikia Chelsea.
EVA (9)
Eva Carneiro na daktari mwenzake Jon Fearn wakiwa kazini.
Aliyekuwa daktari wa timu ya Chelsea, Eva Carneiro (42) amefunga ndoa na mshauri wa biashara aitwaye Jason De Carteret katika Kanisa la St. Patrick jijini London jana.
Eva anakumbukwa sana na mashabiki wa soka kwa kuwa daktari wa Chelsea tangu mwaka 2011 baada ya kupewa nafasi ya kuwa daktari wa kikosi cha kwanza na kocha wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas.
Tangu hapo amefanya kazi na makocha wengine kama Roberto di Matteo, Rafa Benitez hadi alipokuja kusimamishwa kuingia uwanjani na Jose Mourinho mwezi Agosti mwaka huu.
Eva aliingia katika mgogoro na Jose Mourinho baada ya kuingia uwanjani haraka akiwa na daktari mwingine, Jon Fearn kwenda kumtibu Eden Hazard wakati wa pambano kati yao na Swansea na hivyo kuiacha Chelsea ikicheza pungufu ikiwa na wachezaji tisa uwanjani huku ikisaka bao la ushindi.
Katika mchezo huo, Mourinho anaamini kuwa Hazard hakuwa ameumia isipokuwa alikuwa amechoka, hivyo kitendo cha madaktari hao kuingia uwanjani huku tayari kipa Thibaut Courtois akiwa amepewa kadi nyekundu kiliipunguza kasi Chelsea kusaka bao la ushindi.
Katika harusi hiyo hakuna mchezaji yeyote wa Chelsea aliyehudhuria isipokuwa wachezaji wa zamani wa timu hiyo akiwemo kipa Mark Schwarzer ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Leicester City.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
13 Nov 2015

Post a Comment

 
Top