March 14, 2025 02:50:17 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Msanii wa filamu, Vicent Kigosi maarufu kama Ray amekanusha madai kuwa anajichubua.

Ray ameiambia Mpekuzi kuwa anasikitishwa na watu wanaodai kuwa anajichubua bila kujua kuwa mtu akiwa na maisha mazuri anaweza kubadilika.
“Kwanza sijichubui, tatizo unajua baadhi ya watanzania wengi, hawaelewi mimi sijichubui, ila maisha yamebadilika,” amesema.
“Unajua unapokuwa na maisha magumu ya kwanza, unaposhindwa kujikimu, kujinunulia nguo, yaani kufanya unachokitaka kwa muda unaoutaka, unakuwa mweusi kwa sababu huna hela ya kujikimu, sasa unapopata pesa kidogo ya kujikimu, unapokuwa na maisha mazuri , kwako kuna AC, kwenye gari yako kuna AC, hupati jua huwezi kuwa mweusi,” amesisitiza.
“Pia ukishakuwa star lazima muonekano wako uwe tofauti kidogo ili uwe tofauti kidogo. Hawa wanaoona mimi najichubua labla wanaona vibaya! Mimi sijichubui na waache waendelee kuzungumza kwa sababu mtanzania huwezi kumzuia kuzungumza.”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
17 Jul 2015

Post a Comment

 
Top