Mwili wa marehemu ukiwa umepakiwa ndani ya gari ya polisi
Watu wasiojulikana wamemuua mlinzi wa mahakama ya Kingulwira mjini Morogoro kwa kumkata panga kichwani na kunyofoa baadhi ya viungo na kisha kutupa mwili wake katika mashamba ya pangawe mjini Morogoro.
EATV imefika katika eneo hilo na kukuta mwili huo ukiwa umeharibika vibaya huku baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolewa ambapo kwa mujibu wa mashuhuda na ndugu wa marehemu wamesema mtu huyo alipotea nyumbani takribani siku kumi na mbili zilizo pita hadi alipo okotwa na wachunga ng`ombe akiwa ameuawa na mwili wake ukiwa umeharibika.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa tambuka reli Adamu Mwamganga amesema amepata tarifa hizo kwa wachunga ng`ombe kisha kutoa tarifa jeshi la polisi ambapo ameeleza marehemu alikuwa na ugomvi na ndugu zake kuhusu mashamba huenda ndicho chanzo cha kifo chake .
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuuchukua mwili wa marehemu na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti wakati uchunguzi bado unaendelea.
Chanzo:EATV
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment