Mshindi huyo wa ‘Best Live Act’ kwenye MTV MAMA baada ya kurejea Tanzania, amejibu shutuma alizozitoa Jojo dhidi yake kuhusu video aliyoipost, ya mrembo huyo aliyewahi kuwa mpenzi wake akifurahia wimbo wa ‘Mdogo Mdogo’ na kuandika “Mbona Bado, Mtanyooka Tu”.
Kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm, haya ndio majibu ya Diamond kuhusu video aliyoipost na kile alichokiandika Jokate:
“unajua kwanza nimecheka afu nimeskitishwa kwasababu nimeambiwa, sijasoma nimeambiwa kuna post ameandika amezungumzia vitu vingi… Yeye kacheza kama fan wa nyimbo yangu, na mimi nimempost kama fan wangu, ile caption yangu sijamuandika jina kwanini achukulie vibaya?
"Ukiona mtu anajishuku ukiona hivyo kuna namna nyuma. Mbona mi napost watu wengi tu, tena naandika caption zangu za vituko vituko manake mimi nina caption za vituko, mi ni mswahili nimezaliwa Tandale nimekulia Tandale na Tandale ndio kumenifanya leo niwe hapa nilipo…
"kwahiyo nina caption zangu za uswahili kwasababu uswahili ndio umenikuza…siziachi kuziandika mbona naziandikaga katika caption nyingi nyingi kwanini kwake yeye tu aione tatizo, kwani kuna ubaya gani mi kuandika mtanyooka tu kama yeye haimuhusu ina maana labda kuna kitu kinamuhusu.”
Diamond aliendelea:
“Nikaambiwa pia amezungumza kwamba ndio maana wanaogopa kusapoti wasanii watanzania kwasababu akisapoti wanadhalilishwa, yeye mimi mpaka nimeenda kuchukua tuzo hii amenisapoti nini?
"Alipost hata post moja kusema mpigie kura Diamond, afu leo anajishaua eti kanisapoti, kasapoti nini eti kutoa hongera mi nimeshinda tuzo, eti ooh hongera kwa tuzo by the way, angepost kuhamasisha watu wapige kura ili ushindi uje nyumbani, lakini kwa chuki alizojazwa zisizo na sababu na roho mbaya alowekwa na watu imemfanya ashindwe hata kunipost na kutengeneza chuki za chini chini kwa kudhani wakiwapigia kura Wanigeria mi ntakosa tuzo…
"Mungu alivyolaani mi nimeshinda, afu anajifanya anatoa hongera eti wanasapoti muziki wa kiTanzania, utanisapoti nini, lini umenisapoti, au baada ya kuona tuzo imekuja ndo unajifanya kutoa hongera, tuacheni unafiki.” Alimaliza diamond.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Diamond kuwania tuzo 5 za Afrima 2016, Alikiba na Yamoto Band moja08 Sep 20160
Diamond Platnumz ametajwa kuwania vipengele vitano kwenye tuzo za mwaka huu za Afrima. Vipeng...Read more ?
- Busu la Nelly Kamwelu shavuni kwa Diamond akiwa na Wizkid lawatoa povu mashabiki (Video)25 Aug 20160
Haipiti wiki bila Diamond kuwatoa povu mashabiki, hata kama alichokifanya si kwamba alidhamiria...Read more ?
- AUDIO: Kitu Diamond kasema kuhusu yeye kuwa mapenzini na Hamisa Mobetto03 Aug 20160
Ukaribu wako kwenye mitandao ya kijamii siku za karibuni unaweza kuwa ulikukutanisha na stori...Read more ?
- Ujumbe wa Diamond kwa bintiye Wazua Gumzo......Kamwambia "Ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana"23 Jul 20160
Diamond Platnumz si mgeni kwenye jumbe tata kwenye mitandao ya kijamii. Lakini ujumbe wake mpya...Read more ?
- Bifu Kali Kati ya Diamond na Clouds Media23 May 20160
Ni dhahiri sasa msanii wa kimataifa Diamond na brand kubwa ya radio na tv Clouds Fm, bifu la hadh...Read more ?
- Diamond Platnumz: Baada Ya Nape Nnauye Mimi Ndo Waziri wa Habari Na Michezo Mtarajiwa25 Jan 20160
Diamond Platnumz amesema akiachana na muziki anataka kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na ...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment